Headlines

NANI MTANI JEMBE 2, SIMBA, YANGA WAANZA KUTAMBIANA

Posted by Hisia | Jumamosi, 4 Oktoba 2014 | Posted in , ,


Na Mwandishi Wetu
Shindano la ‘Nani Mtani Jembe2’ linalowakutanisha wakongwe wa Soka hapa nchini Simba na Yanga, limeanza kwa kasi msimu huu, baada ya jana kuwepo kwa shamrashamra za aina yake katika uzinduzi rasmi uliofanyika katika viwanja vya Leaders Jijini Dar es Salaam.
Mashabiki lukuki wa timu hizo na viongozi wao jana walijitokeza kwa wingi katika viwanja hivyo katika hafla iliyopambwa na makundi mbalimbali ya timu hizo yaliyokuwa yakitambiana mwanzo mwisho.
Msimu huu wa ‘Nani Mtani Jembe2’ unaoendeshwa na bia ya Kilimanjaro Premium Lager- wadhamini wakuu wa timu hizo, ulishuhudiwa Simba akianza vema katika mchezo wa soka baada ya Mjumbe wake wa Kamati ya Utendaji Said Tully kuwabuziga Yanga bao 1-0 katika mchezo wa kirafiki wa mashabiki wa Simba na Yanga uliokuwa sehemu ya uzinduzi huo.
Katika mchezo huo wa soka ambao ulionekana kuwa na ushindani mkubwa, Simba waliwafunga Yanga iliyoongozwa na nahodha wao Mjumbe wa Kamati ya Utendaji Mohamed Bhinda huku kwa upande wa danadana Bhinda akimshinda Makamu wa Rais wa Simba Geofrey Nyange ‘Kaburu’,huku kwa upande wa 
kuvuta kamba mashabiki wa tiu hizo wakitoka sare.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti viongozi wa timu hizo ‘Kaburu’ wa Simba pamoja na Mohammed Bhinda wa Yanga wote walianza kujigamba kuhakikisha wanaibuka na kitita cha mil 100 ambacho kimeandaliwa na Kilimanjaro Premium Lager.
Kaburu alisema, Yanga wameonekana wazi kuanza kushindwa, baada ya kuwatembezea kichapo cha bao 1-0 na pia kutoka sare ya kuvutana kamba hasa wakizingatia msimu uliopita wa Nani Mtani Jembe waliwazidi katika kila idara isipokuwa katika kura zilizopigwa na mashabiki ambapo Yanga walipigiwa zaidi kura na kuibuka na kitita cha shilingi milioni 98 kati ya milioni 100.
“Hapa imeonekana tumetoka sare katika kuvuta kamba, ila Yanga kama mnavyowajua wanapenda ubishi, wamevuta kamba wengi zaidi ya sisi lakini tumewaachia tu na msimu huu tutahakikisha tunachukua pesa zote na kuwaachia kifuta jasho tu,’alisema Kaburu.
Naye Bhinda aliwataka wanachama na mashabiki wa Yanga kuhakikisha wanaitendea haki Nani Mtani Jembe2 hii ili Yanga iwagalagaze Simba, kwa kuwa msimu uliopita waliwawaonea huruma Simba na kuwapa nafasi ya kuwafunga mabao 3-1 baada ya kuona wamezidiwa katika kuvutana.
“Sisi bwana hatuna shida na hawa watani zetu ndio maana tukawaleta wachezaji kutoka katika kitovu cha soka Brazil na bila ya kuwaleta sisi Simba wangetoa wapi nafasi ya kuwaona Wabrazil wakisakata kabumbu Tanzania,”alisema Bhinda.
Alisema kwa kila bia ya Kilimanjaro Premium Lager yenye ujazo wa milita 500 ambayo mteja atanunua ataona namba maalum na ataandika jina la timu yake (SIMBA au YANGA) ikifuatiwa na namba hiyo na atatuma kwenda namba 15415 na kwa kufanya hivyo atakuwa amepunguza kiasi cha shilingi 10,000 kwenye akaunti ya klabu pinzani na kuiongezea klabu yake kiasi hicho cha sh. 10,000.
“Msimu huu ni wa kipekee sana maana tumeona bora atakayefungwa siku ya mechi ya Nani Mtani Jembe walau apate kifuta jasho cha sh mil 5 huku mshindi akipata milioni 15. Klabu itanufaika, wachezaji watanufaika na mashabiki watanufaika. Sasa ni kazi kwenu viongozi kuwahamasisha mashabiki wa timu zenu,”alisema Kavishe.

NDANDA YAFUGWA GOLI 2 KWA 1 NA COASTAL KATIKA UWANJA WA MKWAKWANI TANGA

Posted by Hisia | | Posted in



 Mchezaji wa timu ya Coastal Union ya Tanga
Mchezaji wa Ndanda Gideon Benson  akitafuta mbinu ya kumtoka Mchezaji wa timu ya Coastal Union ya Tanga Rama Salim wakati wa mechi yao iliyofanyika jijini Tanga Coastal walishinda bao 2.1 Picha









KILIMANJARO PREMIUM LAGER YAKUTANA NA WAHARIRI WA VYOMBO VYA HABARI KUZUNGUMZIA KAMPENI YA “NANI MTANI JEMBE 2”

Posted by Hisia | Ijumaa, 3 Oktoba 2014 | Posted in , ,

Meneja wa Bia ya Kilimanjaro Premium Lager, George Kavishe akizungumza na baadhi ya wahariri wa vyombo habari jijini Dar es Salaam mchana wa leo,wakati wa semina ya kuzungumzia uzinduzi wa Kampeni ya Nani Mtani Jembe sehemu ya 2,utakaofanyika kesho tarehe 4 Oktoba 2014 katika viwanja vya Leaders Club,Kinondoni jijini Dar es salaam. 
Afisa Uhusiano wa Kampuni ya Executive Solutions ambao ndio wanaoratibu Kampeni hiyo ya Nani Mtani Jembe 2,Ibrahim Kyaruzi akizungumza jambo kwenye mkutano huo.
baadhi ya wahariri wa vyombo habari jijini Dar es Salaam wakifatilia kwa makini semina hiyo.
Meneja wa Bia ya Kilimanjaro Premium Lager, George Kavishe akielezea namna Kampeni hiyo itakavyokuwa ikifanyika.

TIMU YA IKULU YA MPIRA WA MIGUUYATINGA HATUA YA PILI SHIMIWI.

Posted by Hisia | Alhamisi, 2 Oktoba 2014 | Posted in

01Wachezaji wa timu ya Ikulu wakiwa pamoja kuomba dua kabla ya kuanza mchezo wao dhidi ya timu ya RAS Simiyu katika mashindano ya SHIMIWI leo uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro.
02
03
04Wachezaji wa timu ya Ikulu wakifanya mazoezi mbalimbali kabla ya kuanza mchezo wao dhidi ya timu ya RAS Simiyu katika mashindano ya SHIMIWI leo uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro.
05 
Kikosi kamili cha timu ya Ikulu kikiwa katika picha ya pamoja.
06
07
08
09 
Picha ya pamoja ya wachezaji na viongozi wa timu ya mpira wa miguu ya Ikulu inayoshiriki mashindano ya SHIMIWI mjini Morogoro.
Na Eleuteri Mangi-MAELEZO 02/10/2014 Timu ya mpira wa miguu ya Ikulu imedhihirisha ubora wake katika mashindano ya Shirikisho la Michezo ya watumishi inayoshirikisha Wizara na Idara za Serikali (SHIMIWI) kwa kumaliza mechi nne katika kundi B bila kuruhusu nyavu zake kutikiswa. Ubora huo unaifanya timu ya Ikulu kuwa ni timu iliyojihakikishia kuendelea katika mzunguko wa pili katika mashindano hayo ambapo unashirikisha timu 32 zitakazofuzu kuingia mzunguko huo. Hatua hiyo imeifanya timu ya Ikulu iwe na siku njema ambayo imeonekana asubuhi ya leo mjini Morogoro. Hivyo ndivyo ilivyokuwa kwa timu ya mpira wa miguu ya Ikulu inayoshiriki mashindano ya SHIMIWI yanayoendelea leo mjini Morogoro katika viwanja mbalimbali. Siku imekuwa njema kwa timu hiyo kwa kuwa timu pinzani waliokuwa wacheze nao kutokutokea uwanja wa Jamhuri ambapo ilikuwa ichezwe mechi hiyo dhidi ya RAS Simiyu. Baada ya kutokutokea uwanjani hapo mwamuzi wa mchezo huo alikagua timu ya Ikulu na kuwaingiza uwanjani kwa dakika 25 akingojea kama Simiyu watatokea. Baada ya muda huo kuisha, mwamuzi akizingatia kanuni za mashindano hayo aliamuru timu ya Ikulu wapewe pointi tatu (3) na magoli mawili (2) ya ushindi kwa kufika uwanjani hapo. Timu hiyo sasa imefikisha pointi 10 na magoli sita 6 ya kufunga ambayo timu za kundi B hakuna itakayofikisha pointi hizo hadi sasa. Kikosi cha timu ya mpira wa miguu Ikulu kinaongozwa na mwalimu George Mbilinyi na daktari wa timu Nassoro nAlli ambapo kwa upande wa wachezaji kinaundwa na William Niva, Kigan Kyando, Abdallah Omari, Jeriko Masebo, Michael Marekana, Meeda Absalom, Sande Chilunda, Hakimu Ambari, Salehe Hamadi, Samuel Grayson na Abrahaman Almasi. Wachezaji wengine ni Rajabu Mbaga, Mrisho Mihambo, Amos Ndege, Robert Petro, Samuel Shisha, Erick Kafuku na Nassoro Alli. Kundi B katika mashindano ya SHIMIWI linaundwa na timu ya Ikulu, Wizara ya Afya na Ustawi wa jamii, Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Uhamiaji, na RAS Simiyu.

PHIRI AELEZA ANAVYOUMIZWA NA SARE MBILI ZA SIMBA

Posted by Hisia | | Posted in ,


Kocha wa Simba, Patrick Phiri amesema yeye na benchi lake la ufundi wanaumiza kichwa sana ili kubadilisha mambo kadhaa.

Phiri raia wa Zambia amesema yeye na wenzake wamekuwa wakifanya kazi kwa nguvu kurekebisha mambo.

"Kuanza kuamini sasa Simba imefanya vibaya haitakuwa sawa, lakini kuamini tunachofanya sasa ni sawa, pia sio sahihi.
"Ndiyo maana tunafanya kazi kwa juhudi kubadilisha hali hii na imani ni kubwa tutabadili mambo na kuanza kufanya vema.
"Hakuna anayeweza kufurahia hali hii, mashabiki na viongozi lakini si hali nzuri kwetu. Hivyo tunaendelea kupambana," alisema Phiri ambaye ni mtaratibu.
Simba imecheza mechi mbili za mwanzo za Ligi Kuu Bara na kutoka sare mbili.

Hali hiyo inaonekana kuwaudhi mashabiki wa Simba na wengi wao wamekuwa wakitamani kuiona angalau inapata ushindi wa kwanza kwenye Ligi Kuu Bara.

MASHABIKI WA GALATASARAY WAKINUKISHA DIMBANI EMARATES, SITA KATI YAO KIZUIZINI KWA UCHUNGUZI ZAIDI.

Posted by Hisia | | Posted in


Huenda adhabu kali kutoka UEFA  ikawapata mashabiki wa klabu ya Galatasaray kwa kutupa mafataki (flares) uwanjani wakati wa mechi yao dhidi ya Arsenal, mchezo ambayo ulipigwa katika dimbani la Emarates na Arsenal kuibuka na ushindi wa magoli 4-1 dhidi ya klabu hiyo ya Galatasaray  yenye makazi yake jijini Instanbul nchini Uturuki.

One Galatasaray fan gives the finger as the fans around him go wild amid the billowing smoke
Usiombe kukutana na mashabiki wa Galatasaray, mwangali huyo shabiki mmoja Galatasaray akiporomosha litusi la kidole kwa wachezaji wa Arsenal huku wenzake wakimshangilia
Fernando Muslera removes one of the flares during the Champions League clash - Danny Welbeck had struck a double to put the Gunners in front
Pichani ni mlinda lango wa Galatasaray, Fernando Muslera akijaribu kuondoa moja ya fataki iliyorushwa uwanjani na mashabiki wa timu  yake.
Mashabiki wa Galatasaray ambao wanasifika kwa uzalendo mkubwa walionao na timu yao hiyo, walianza kurusha mafataki ndani ya uwanja dakika ya 36 ya mchezo, mara baada ya kuona timu yao imezidiwa na Arsenala baada ya timu hiyo kuwa mbele kipindi cha kwanza kwa magoli 2-0, magoli ambayo yalifungwa na mshambuliaji wa zamani wa Manchester United, Danny Welbeck.

Police were deployed at the end to try and prevent a repeat of the scenes in the first half
Ilikuwa ni shughuli pevu kwa upande wa maafisa wa usalama kuwatuliza mashabiki hao dimbani Emarates. Mpaka hivi sasa watu sita wanashikiliwa rumande kwa tuhuma za kuhusika na usumbufu huo.
Hata hivyo hamsha hamsha hiyo ya mashabiki ambao ulifanya mchezo usimame kwa dakika kadhaa, iliweza kuthibitiwa mara moja na ma-afisa usalama waliokuwepo uwanjani hapo ingawaje mashabiki wa Galatasaray baadaye waliendelea kupiga mafataki hayo nje ya uwanja wa Emarates baada ya mtanange huo.

Kwa upande wa idara ya nidhamu ya UEFA, imesema itachukua hatua stahiki kwa mashabiki hao kwani ni kosa kisheria kutupa vitu ndani ya unja wakati wa mchezo.

Mbali na kuwa na heshima kubwa, mashindano ya Mabingwa barani Ulaya (CL) huwa na faida kubwa sana kwa klbu kwani ni moja ya ligi inayotoa pesa nyingi kwa timu shiriki halikadhalika kwa timu itakayo nyakuwa ubingwa

RAIS WA TFF AWEKA MAMBO BAYANA KUHUSU KAMATI YA UTENDAJI YA TFF NA BODI YA LIGI

Posted by Hisia | | Posted in

Vyombo kadhaa vya habari vimeripoti kuhusu hali ya mgongano kati ya Kamati ya Utendaji ya TFF na Bodi ya ligi Tanzania (Tanzania Premier league Board).
Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania linapenda kutoa ufafanuzi ufuatao:

1.Bodi ya ligi imeundwa kwa mujibu wa Katiba ya TFF kifungu 40(11).Hivyo Bodi ya ligi ni zao la Mkutano Mkuu wa TFF.
2.Katiba ya TFF imeipa mamlaka  kamati ya utendaji ya TFF kutunga kanuni za uendeshaji wa Bodi ya ligi,kanuni hizi ndiyo nguzo kuu ya uendeshaji wa shughuli za Bodi ya ligi na ndizo zinaipa Bodi uhalali wake wa kuendesha shughuli zake za kila siku.
3.Bodi ya ligi ni chombo cha TFF kama vilivyo vyombo vingine vikiwemo kamati mbali mbali za TFF.Kisheria Bodi ya ligi sio chombo huru (its not a legal entity) hivyo Bodi pamoja na mambo mengine haina mamlaka ya kuingia mikataba ya aina yoyote ya kisheria .
4.Katiba ya TFF inatamka kuwa Bodi ya ligi itaheshimu na kufuata maagizo ya TFF.Maagizo haya yanatolewa na Sekretarieti ya TFF kwa niaba ya  kamati ya utendaji ya TFF.
5.Mwenye mamlaka ya kutengua maamuzi ya kamati ya utendaji ya TFF ni Mkutano Mkuu wa TFF peke yake,hakuna chombo kingine cha chini chenye mamlaka hayo.
6.Kanuni za mashindano zinaandaliwa na kamati ya mashindano ya TFF na kupitishwa na kamati ya utendaji ya TFF. Kikao cha kamati ya utendaji kilichopitisha rasimu ya kanuni za ligi za mwaka 2014/15 kilihudhuriwa na Mwenyekiti wa bodi ya  ligi,Makamu mwenyekiti  wa Bodi ya ligi na pia Mwenyekiti wa kamati ya mashindano ya TFF,hawa wote ni wajumbe wa Bodi ya ligi na walishiriki kikamilifu katika kikao cha kamati ya utendaji kilichopitisha kanuni za ligi 2014/15 ukiwemo na utaratibu wa mgawanyo wa mapato ya milangoni na ya udhamini.Katiba ya TFF inaagiza hivyo kuwa Viongozi wakuu wa Bodi ya ligi watakuwa  pia ni wajumbe wa kamati ya utendaji ya TFF. Aidha mtendaji mkuu wa Bodi ya ligi alikuwepo kwenye kikao hiki cha kamati ya utendaji  kama mwajiriwa.
7. Uamuzi wa kuunda mfuko maalum wa kuendeleza soka la vijana ni uamuzi uliopitishwa na kamati ya utendaji.Lengo la kuanzishwa mfuko huu ni kuwa na chombo maalum ambacho kitakuwa kinakusanya fedha toka vyanzo mbali mbali kwa ajili ya kuendeleza miradi ya soka la vijana nchini.Kwa sasa miradi hii ni:
(a) Kuanzisha vituo vya kulea na kuendeleza vipaji vya watoto kuanzia miaka 8-17  (sports centres) katika kila mkoa nchini mwetu.Mradi huu ni mkubwa utahitaji nyenzo hasa walimu na vifaa.
(b) Kuandaa timu ya taifa umri chini ya miaka 12  kwa ajili ya mashindano ya Afrika umri chini ya miaka 17 mwaka 2019. Timu hii itaanza kuandaliwa mwaka huu Desemba baada ya mashindano ya kitaifa umri chini ya miaka 12. Hii timu itakusanywa na kuwekwa katika shule moja ya bweni ambapo watalelewa na kuendelezwa vipaji vyao wakiwa pamoja huku wanasoma.Tanzania tumeomba kuwa wenyeji wa fainali hizi.
(c) Kuandaa timu ya Taifa umri chini ya miaka 14 kwa ajili ya michuano ya awali mwaka 2016 kuelekea fainali za Afrika umri chini ya miaka 17 mwaka 2017.
(d) Kuandaa timu ya Taifa umri chini ya miaka 17 kwa ajili ya michuano ya awali mwaka 2016 kuelekea fainali za Afrika umri chini ya miaka 20 mwaka 2017.
(e) Kuandaa mashindano ya Taifa ya mpira wa wanawake na ligi ya taifa ya mpira wa wanawake.
Miradi yote hii muhimu kwa maendeleo ya mpira wa miguu Tanzania haina udhamini lakini ni lazima ifanyike ili tujihakikishie tunainua mpira nchini mwetu.Mafanikio ya miradi hii sio tu yatafaidisha na kuimarisha timu zetu za Taifa lakini pia yatakuwa chimbuko madhubuti la wachezaji mahiri wa vilabu vyetu vya mpira wa miguu.
Kimsingi tunatarajia kuwa vyanzo vikuu vya mapato ya kutunisha mfuko wa maendeleo ya mpira Tanzania vitakuwa:
-          Mapato yatokanayo na mechi za ligi zetu madaraja yote
-          Mapato yatokanayo na mechi za kimataifa
-          Wadhamini
-          Serikali kuu kupitia bajeti za Wizara zenye dhamana ya michezo,halmashauri na vyuo
-          Wafadhili
-          Shughuli mbali mbali za kutunisha mfuko.
Kamati ya utendaji ya TFF ilimteua Bwana Leodeger Tenga kuwa mwenyekiti wa kwanza wa mfuko huu na wajumbe wake ni Bw Tarimba Abbas, Bw Ephraim Mafuru, Mzee Ayoub Chamshama Bw Frederick Mwakalebela na Mh Zarina Madabida. Bw Henry Tandau na Bw Boniface Wambura ni waratibu wa mfuko huu. Imani ya TFF ni kuwa wajumbe hawa kwa kutumia uzoefu wao katika uongozi wa jamii watatusaidia kuhakikisha mfuko huu unaanza vyema shughuli zake.
Upande wa TFF tumefungua akaunti maalum benki kwa ajili ya kuingiza fedha zote zinazokusanywa kama mchango wa TFF kwenye mfuko huu zikiwemo asilimia 5 za makato ya fedha za udhamini na ZILE zitokanazo na mfuko wa jichangie,TFF inatoa wito kwa wadau wote wa mpira wa miguu Tanzania kuchangia mfuko huu ili utumike kunusuru mpira wetu. Fedha zitakazokusanywa matumizi yake yatasimamiwa na kanuni za uendeshwaji wa mfuko huu.

Hitimisho:
Kila mwanafamilia wa TFF  anawajibika kuheshimu na kufuata maelekezo ya Kanuni za mashindano ya ligi kuu kama zilivyopitishwa na Kamati ya Utendaji ya TFF .Hivyo  utaratibu wa mgawanyo wa mapato yatokanayo na fedha za milangoni na za wadhamini kama ulivyoainishwa kwenye kanuni hizi uko pale pale. Ninaiagiza Bodi ya ligi kusimamia utekelezaji wa maagizo ya Kamati ya utendaji ya TFF mara moja. Mwenye malalamiko kuhusu  kanuni hizi ayalete kwenye vyombo husika  vya TFF kwa kufuata Katiba,kanuni na taratibu za Shirikisho.Sote tunajenga nyumba moja hakuna haja ya kugombea fito.

Jamal Malinzi
Rais wa TFF
Dar es salaam

02/October/2014

MADRID YASHINDA KWA MBINDE, RONALDO AKOSA PENALTI, ATLETICO YAITULIZA JUVE - MATOKEO YOTE YAPO HAPA

Posted by Hisia | | Posted in , , , ,



Real Madrid imelazimika kufanya kazi ya ziada kushinda kwa mabao 2-1 dhidi ya timu kibonde ya Ludogoret.

Mabao ya Madrid katika mechi hiyo ya Ligi ya Mabingwa Ulaya hatua ya makundi yalifungwa na Cristiano Ronaldo kwa mkwaju wa penalti lakini ikiwa ni baada ya kukosa mkwaju wa kwanza, Madrid ilipata mikwaju miwili ya penalti.
Bao la pili na la ushindi lilifungwa na mshambuliaji Mfaransa, Karim Benzema.

Katika mechi nyingine, Atletico Madrid ikiwa nyumbani, imeituliza Juventus ya Italia kwa kuitwanga kwa bao 1-0, muuaji akiwa ni Mturuki, Arda Turan, kama unamkubuka ndiyo yule aliyeiua Real Madrid.

MATOKEO MENGINE LEO:
Zenit 0-0 Monaco
B. Leverkusen 3-1 Benfica
Anderlecht 0-3 Borussia Dortmund
Malmo 2-0 Olimpiakos

RONALDO BADO MABAO MAWILI TU KUMKAMATA RAUL LIGI YA MABINGWA, MESSI ATUPWA HUKO!

Posted by Hisia | | Posted in

BADO mabao mawili tu Cristiano Ronaldo afikie idadi ya mabao ya Raul anayeongoza kwa kufunga zaidi kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya. 
Ronaldo usiku huu amezidi 'kuisuuza roho' ya kocha wake, Carlo Ancelotti baada ya kufunga bao moja katika ushindi wa 2-1 ugenini dhidi ya PFC Ludogorets Razgrad.
Wenyeji walitangulia kupata bao dakika ya sita kupitia kwa Marcelinho kabla ya Cristiano Ronaldo kufunga kwa penalti na Karim Benzema kufunga la ushindi kwa Real Madrid.
Mfalme wa mabao; Nyota wa Real Madrid, Cristiano Ronaldo amebakiza bao moja kufikia rekodi ya Raul katika Ligi ya Mabingwa Ulaya

WAFUNGAJI BORA WA KIHISTORIA LIGI YA MABINGWA UALAYA 

1. Raul - Mabao 71 
2. Cristiano Ronaldo - Mabao 69
2= Lionel Messi - Mabao 68
4. Ruud van Nistelrooy - Mabao 56
5. Thierry Henry - Mabao 50
6. Alfredo Di Stefano - Mabao 49
7. Andriy Shevchenko - Mabao 48
8. Eusebio - Mabao 46
8= Filippo Inzaghi - Mabao 46 
10. Didier Drogba - Mabao 42 
Mwanasoka huyo bora wa dunia sasa anatimiza mabao 69 aliyofunga katika Ligi ya Mabingwa Ulaya, mawili nyuma ya Raul aliyefunga mara 71.
Anafunga bao hilo siku moja baada ya kocha Ancelotti kukaririwa akisema "Ni mchezaji bora zaidi niliyewahi kumfundisha,".
Kipenzi huyo wa mashabiki wa Manchester United sasa anamzidi kwa bao moja, mpinzani wake Lionel Messi wa Barcelona, ambaye ana mabao 68. Ruud van Nisterlooy anashika nafasi ya nne kwa mabao yake 56, Thierry Henry mwenye mabao 50 ni wa tano, Alfred de Stefano mwenye mabao 49 ni wa sita, Andriy Shevchenko mwenye mabao 48 ni wa saba, wakati Eusebio mwenye mabao 46 sawa na Filippo Inzaghi wanashika nafasi ya nane. Didier Drogba anakamilisha orodha ya wachezaji 10 waliofunga mabao mengi Ligi ya Mabingwa kwa mabao yake  42.

ARSENAL YAUA, WELBECK AGONGA HAT-TRICK

Posted by Hisia | | Posted in

Mshambuliaji Danny Welbeck akishangilia baada ya kupiga 'hat-trick'.
Alexis Sanchez akiifungia Arsenal bao la tatu dhidi ya Galatasaray.
Welbeck akitupia bao la nne.
Kocha wa Arsenal, Arsene Wenger ametimiza miaka 18 akiwa meneja wa klabu hiyo leo.
KLABU ya Arsenal imetoa kichapo cha mabao 4-1 dhidi ya Galatasaray kwenye mechi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya iliyopigwa Uwanja wa Emirates jijini London usiku huu.
Mshambuliaji Danny Welbeck ametupia kambani mabao matatu 'hat-trick' huku bao la nne likiwekwa kimianai na Alexis Sanchez. Katika mtanange huo, kipa wa Arsenal, Wojciech Szczesny alizawadiwa kadi nyekundu baada ya kumfanyia madhambi mshambuliaji wa Galatasaray, Burak Yilmaz.
Ushindi wa leo wa Arsenal umeongeza furaha kwa Meneja wa timu hiyo, Arsene Wenger aliyetimiza miaka 18 akiwa kocha wa klabu hiyo leo.
VIKOSI:
Arsenal: Szczesny, Chambers, Mertesacker, Koscielny, Gibbs, Flamini, Cazorla, Ozil (Wilshere 77), Sanchez (Ospina 62), Oxlade-Chamberlain (Rosicky 68), Welbeck.
Waliokuwa benchi: Coquelin, Bellerin, Campbell, Podolski.

Galatasaray: Muslera, Chedjou, Felipe Melo, Semih Kaya, Veysel (Bulut 68), Yekta (Altintop 46), Dzemaili, Telles, Sneijder, Pandev (Bruma 68), Burak Yılmaz.
Waliokuwa benchi: Bolat, Balta, Adin, Camdal.

MPAMBANO WA NGUMI KUPIGWA SIKU YA NYERERE DAY TANDIKA

Posted by Hisia | Jumatano, 1 Oktoba 2014 | Posted in

Na Mwandishi Wetu

BONDIA Imani Daudi anatarajia kupigan
a na Patrick  Amote kutoka kenya kwenye mpambano wa kimataifa wa mchezo wa masumbwi utakaofanyika katika ukumbi wa musoma bar Tandika siku ya kumbukumbu ya baba wa Taifa Nyerere Day tarehe 14 mwezi huu mpambano huo unaoratibiwa na oganaizesheni ya ngumi za kulipwa nchini TPBO chini ya Rais wake Yassin Abdallah 'Osthadhi'

lina marengo ya kumkumbuka baba wa taifa katika siku hiyo ya kipekee kabisa kwa nchi yetu ya Tanzania

akizungumza na mwandishi wa habari hizi Abdallah amesema kuwa kila mwaka wanafanya hivyo kwa ajili ya kumkumbuka baba wa taifa hili ambaye alipenda michezo mbalimbali bila ubaguzi wa aina yoyote hile ingawa kwa sasa michezo inabaguliwa kwa mingine kupewa ufadhili na mingine kupewa kidogo na mingine kunyimwa kabisa ufadhili

aliongeza kuwa siku hiyo pia kutakuwa na mipambano mbalimbali ya utangulizi moja likiwa bondia Shomari Milundi atamenyana na Suma Ninja na mapambano mengine mbalimbali

nae bondia Imani Daudi amejidhatiti kufanya kweli kwa kumsambalatisha Amote wa kenya ili aendeleze wimbi lake la ushindi na kuvutia mashabiki zaidi katika mchezo huo wa masumbwi

siku hiyo pia kutakuwa zikiuzwa DVD mpya za masumbwi ambazo zinaonesha mafunzo mbalimbali ya mchezo wa ngumi yanavyoanza hatua kwa hatua

mpaka kujua kitu kamili katika


mchezo huo pia kunakuwa na mapambano ya mabondia mabigwa wa dunia wa mchezo huo kama Floyd

Maywether, Manny Paquaio,mike Tyson, Mohamed Alli pamoja na mabambano ya ngumi ya ndani

PENALTI TATA YAIPA BAYER MUNICH USHINDI DHIDI YA CSKA MOSCOW - mechi yachezwa bila watazamaji, rungu la UEFA lawaadhibu Warusi

Posted by Hisia | | Posted in ,


CSKA Moscow goalkeeper Igor Akinfeev dives right as Bayern's Muller lifts the ball down the centre of the net
THOMAS Mueller amefunga kwa njia ya penalti na kuipatia Bayern Munich ushindi wa 1-0 kwenye uwanja wa ugenini Arena Khimki dhidi ya CSKA Moscow.
Mabingwa hao wa Ujerumani walibanwa na kujikuta wakihitaji penalti utata ili kuzoa pointi tatu muhimu.
Muller gave Bayern Munich the important lead in front of a virtually empty Luzhniki Stadium on Tuesday night
Kiungo Mario Goetze alionekana kufanyiwa faulo na Mario Fernandes nje ya box lakini mwamuzi Willie Collum kutoka Scotland akaamuru penalti iliyozaa goli dakika ya 22.
Robert Lewandowski of Bayern Munich wins a header during the Champions League Group E match 
Mchezo huo wa kundi E ulichezwa bila watazamaji baada ya baada ya UEFA kulazimika kuwaadhibu mabingwa hao wa Urusi kwa kitendo cha mashabiki wao kuimba nyimbo za kibaguzi katika mchezo wao dhidi ya Viktoria Plzen mwezi Disemba mwaka jana.
Arjen Robben of Bayern Munich escapes the challenge of Ahmed Musa of CSKA Moscow on Tuesday night
CSKA Moscow XI: Akinfeev, Mario Fernandes, Vasili Berezutski, Ignashevich, Shchennikov, Alexsei Berezutski, Tosic (Efremov 78), Natcho (Doumbia 66), Eremenko, Milanov, Musa
Bayern Munich XI: Neuer, Benatia, Dante, Alaba, Robben (Rafinha 81), Lahm, Alonso, Bernat, Gotze (Shaqiri 77), Muller, Lewandowski (Pizarro 90).