Published On:Jumatano, 1 Oktoba 2014
Posted by Hisia
PENALTI TATA YAIPA BAYER MUNICH USHINDI DHIDI YA CSKA MOSCOW - mechi yachezwa bila watazamaji, rungu la UEFA lawaadhibu Warusi
THOMAS
Mueller amefunga kwa njia ya penalti na kuipatia Bayern Munich ushindi
wa 1-0 kwenye uwanja wa ugenini Arena Khimki dhidi ya CSKA Moscow.
Mabingwa hao wa Ujerumani walibanwa na kujikuta wakihitaji penalti utata ili kuzoa pointi tatu muhimu.
Kiungo Mario Goetze
alionekana kufanyiwa faulo na Mario Fernandes nje ya box lakini mwamuzi
Willie Collum kutoka Scotland akaamuru penalti iliyozaa goli dakika ya
22.
Mchezo
huo wa kundi E ulichezwa bila watazamaji baada ya baada ya UEFA
kulazimika kuwaadhibu mabingwa hao wa Urusi kwa kitendo cha mashabiki
wao kuimba nyimbo za kibaguzi katika mchezo wao dhidi ya Viktoria Plzen mwezi Disemba mwaka jana.
CSKA
Moscow XI: Akinfeev, Mario Fernandes, Vasili Berezutski, Ignashevich,
Shchennikov, Alexsei Berezutski, Tosic (Efremov 78), Natcho (Doumbia
66), Eremenko, Milanov, Musa
Bayern
Munich XI: Neuer, Benatia, Dante, Alaba, Robben (Rafinha 81), Lahm,
Alonso, Bernat, Gotze (Shaqiri 77), Muller, Lewandowski (Pizarro 90).