Published On:Alhamisi, 2 Oktoba 2014
Posted by Hisia
TIMU YA IKULU YA MPIRA WA MIGUUYATINGA HATUA YA PILI SHIMIWI.
Wachezaji
wa timu ya Ikulu wakiwa pamoja kuomba dua kabla ya kuanza mchezo wao
dhidi ya timu ya RAS Simiyu katika mashindano ya SHIMIWI leo uwanja wa
Jamhuri mjini Morogoro.
Wachezaji
wa timu ya Ikulu wakifanya mazoezi mbalimbali kabla ya kuanza mchezo
wao dhidi ya timu ya RAS Simiyu katika mashindano ya SHIMIWI leo uwanja
wa Jamhuri mjini Morogoro.
Kikosi kamili cha timu ya Ikulu kikiwa katika picha ya pamoja.
Picha ya pamoja ya wachezaji na viongozi wa timu ya mpira wa miguu ya Ikulu inayoshiriki mashindano ya SHIMIWI mjini Morogoro.
Na Eleuteri Mangi-MAELEZO
02/10/2014
Timu ya mpira wa miguu ya Ikulu imedhihirisha ubora wake katika
mashindano ya Shirikisho la Michezo ya watumishi inayoshirikisha Wizara
na Idara za Serikali (SHIMIWI) kwa kumaliza mechi nne katika kundi B
bila kuruhusu nyavu zake kutikiswa.
Ubora huo unaifanya timu ya Ikulu kuwa ni timu iliyojihakikishia
kuendelea katika mzunguko wa pili katika mashindano hayo ambapo
unashirikisha timu 32 zitakazofuzu kuingia mzunguko huo.
Hatua hiyo imeifanya timu ya Ikulu iwe na siku njema ambayo imeonekana asubuhi ya leo mjini Morogoro.
Hivyo ndivyo ilivyokuwa kwa timu ya mpira wa miguu ya Ikulu
inayoshiriki mashindano ya SHIMIWI yanayoendelea leo mjini Morogoro
katika viwanja mbalimbali.
Siku imekuwa njema kwa timu hiyo kwa kuwa timu pinzani waliokuwa
wacheze nao kutokutokea uwanja wa Jamhuri ambapo ilikuwa ichezwe mechi
hiyo dhidi ya RAS Simiyu.
Baada ya kutokutokea uwanjani hapo mwamuzi wa mchezo huo
alikagua timu ya Ikulu na kuwaingiza uwanjani kwa dakika 25 akingojea
kama Simiyu watatokea.
Baada ya muda huo kuisha, mwamuzi akizingatia kanuni za
mashindano hayo aliamuru timu ya Ikulu wapewe pointi tatu (3) na magoli
mawili (2) ya ushindi kwa kufika uwanjani hapo.
Timu hiyo sasa imefikisha pointi 10 na magoli sita 6 ya kufunga
ambayo timu za kundi B hakuna itakayofikisha pointi hizo hadi sasa.
Kikosi cha timu ya mpira wa miguu Ikulu kinaongozwa na mwalimu
George Mbilinyi na daktari wa timu Nassoro nAlli ambapo kwa upande wa
wachezaji kinaundwa na William Niva, Kigan Kyando, Abdallah Omari,
Jeriko Masebo, Michael Marekana, Meeda Absalom, Sande Chilunda, Hakimu
Ambari, Salehe Hamadi, Samuel Grayson na Abrahaman Almasi.
Wachezaji wengine ni Rajabu Mbaga, Mrisho Mihambo, Amos Ndege, Robert Petro, Samuel Shisha, Erick Kafuku na Nassoro Alli.
Kundi B katika mashindano ya SHIMIWI linaundwa na timu ya Ikulu,
Wizara ya Afya na Ustawi wa jamii, Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni
na Michezo, Uhamiaji, na RAS Simiyu.