Huenda adhabu kali kutoka UEFA ikawapata mashabiki wa klabu ya Galatasaray kwa kutupa mafataki
(flares) uwanjani wakati wa mechi yao dhidi ya Arsenal, mchezo ambayo
ulipigwa katika dimbani la Emarates na Arsenal kuibuka na ushindi wa
magoli 4-1 dhidi ya klabu hiyo ya Galatasaray yenye makazi yake jijini
Instanbul nchini Uturuki.
|
Usiombe
kukutana na mashabiki wa Galatasaray, mwangali huyo shabiki mmoja
Galatasaray akiporomosha litusi la kidole kwa wachezaji wa Arsenal huku
wenzake wakimshangilia |
|
Pichani ni mlinda lango wa Galatasaray, Fernando Muslera akijaribu kuondoa moja ya fataki iliyorushwa uwanjani na mashabiki wa timu yake. |
Mashabiki wa Galatasaray ambao wanasifika kwa uzalendo mkubwa walionao
na timu yao hiyo, walianza kurusha mafataki ndani ya uwanja dakika ya 36
ya mchezo, mara baada ya kuona timu yao imezidiwa na Arsenala baada ya
timu hiyo kuwa mbele kipindi cha kwanza kwa magoli 2-0, magoli ambayo
yalifungwa na mshambuliaji wa zamani wa Manchester United, Danny
Welbeck.
|
Ilikuwa ni
shughuli pevu kwa upande wa maafisa wa usalama kuwatuliza mashabiki hao
dimbani Emarates. Mpaka hivi sasa watu sita wanashikiliwa rumande kwa
tuhuma za kuhusika na usumbufu huo. |
Hata hivyo hamsha hamsha hiyo ya mashabiki ambao ulifanya mchezo usimame
kwa dakika kadhaa, iliweza kuthibitiwa mara moja na ma-afisa usalama
waliokuwepo uwanjani hapo ingawaje mashabiki wa Galatasaray baadaye
waliendelea kupiga mafataki hayo nje ya uwanja wa Emarates baada ya mtanange huo.
Kwa upande wa idara ya nidhamu ya UEFA, imesema itachukua hatua stahiki
kwa mashabiki hao kwani ni kosa kisheria kutupa vitu ndani ya unja
wakati wa mchezo.
Mbali na kuwa na heshima kubwa, mashindano ya Mabingwa barani Ulaya (CL)
huwa na faida kubwa sana kwa klbu kwani ni moja ya ligi inayotoa pesa
nyingi kwa timu shiriki halikadhalika kwa timu itakayo nyakuwa ubingwa
About the Author
Posted by Hisia
on 10/02/2014 05:05:00 PM. Filed under
Uingereza
.
You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0.
Feel free to leave a response
By Hisia
on 10/02/2014 05:05:00 PM. Filed under
Uingereza
.
Follow any responses to the RSS 2.0. Leave a response