Published On:Alhamisi, 2 Oktoba 2014
Posted by Hisia
RONALDO BADO MABAO MAWILI TU KUMKAMATA RAUL LIGI YA MABINGWA, MESSI ATUPWA HUKO!
BADO
mabao mawili tu Cristiano Ronaldo afikie idadi ya mabao ya Raul
anayeongoza kwa kufunga zaidi kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Mfalme wa mabao; Nyota wa Real Madrid, Cristiano Ronaldo amebakiza bao moja kufikia rekodi ya Raul katika Ligi ya Mabingwa Ulaya
Ronaldo
usiku huu amezidi 'kuisuuza roho' ya kocha wake, Carlo Ancelotti baada
ya kufunga bao moja katika ushindi wa 2-1 ugenini dhidi ya PFC
Ludogorets Razgrad.
Wenyeji
walitangulia kupata bao dakika ya sita kupitia kwa Marcelinho kabla ya
Cristiano Ronaldo kufunga kwa penalti na Karim Benzema kufunga la
ushindi kwa Real Madrid.
Mwanasoka
huyo bora wa dunia sasa anatimiza mabao 69 aliyofunga katika Ligi ya
Mabingwa Ulaya, mawili nyuma ya Raul aliyefunga mara 71.
Anafunga bao hilo siku moja baada ya kocha Ancelotti kukaririwa akisema "Ni mchezaji bora zaidi niliyewahi kumfundisha,".
Kipenzi
huyo wa mashabiki wa Manchester United sasa anamzidi kwa bao moja,
mpinzani wake Lionel Messi wa Barcelona, ambaye ana mabao 68. Ruud van
Nisterlooy anashika nafasi ya nne kwa mabao yake 56, Thierry Henry
mwenye mabao 50 ni wa tano, Alfred de Stefano mwenye mabao 49 ni wa
sita, Andriy Shevchenko mwenye mabao 48 ni wa saba, wakati Eusebio
mwenye mabao 46 sawa na Filippo Inzaghi wanashika nafasi ya nane. Didier
Drogba anakamilisha orodha ya wachezaji 10 waliofunga mabao mengi Ligi
ya Mabingwa kwa mabao yake 42.