Published On:Jumatatu, 8 Septemba 2014
Posted by Hisia
LIONEL MESSI AMGARAGAZA CRISTIANO RONALDO TUZO YA FIFA 15, LIGI KUU ENGLAND YACHEMSHA KINOMA!
Mcheza bora wa dunia: EA Sports wamemuweka nyota wa Barcelona, Lionel Messi kuwa namba moja katika michezo mipya ya FIFA 15
CRISTIANO Ronaldo alimgaragaza Lionel
Messi katika tuzo ya Ballon d'Or mapema mwaka huu,lakini nyota huyo wa
Barcelona amelipa kisasi kwa mpinzani wake huyo mkubwa kwa kushinda tuzo
nyingine.
Akiwa amepata pointi 93 kati ya 100,
messi amekuwa namba moja katika tuzo ya michezo ya Video ya FIFA, (FIFA
15) ambayo itatangazwa rasmi septemba 26 mwaka huu huko UK.
Ili kuwapa nafasi mashabiki kupiga kura kabla, waendeshaji wa tuzo hiyo, EA Sports walitangaza majina ya wachezaji 50.
Mtu anayetakiwa: Barcelona watakuwa
maarufu zaidi katika michezo mipya ya Video baada ya Messi kuibuka
kinara kwa takwimu za sasa.
Namba mbili: Nyota wa Real Madrid, Cristiano Ronaldo amepewa pointi 92 katika tuzo ya FIFA 15
Hatari: EA Sports wameupa uwezo wa Ronaldo wa kupiga mashuti pointi 93 kati ya 100.
Messi amemshinda Ronaldo kwa tofauti ya pointi moja nyota wa Real Madrid aliyepata alama 92 hasa katika uwezo wa kufunga mabao.
Nyota wa Bayern Munich na Uholanzi Arjen Robben ameshika namba tatu kwa pointi zake 90.
Takwimu hizo zinazozingatia zaidi
kiwango cha mchezaji katika mechi za ligi na makombe katika siku 365
zilizopita, zinaonesga uwezo wa kila mchezaji kila anapotumika katika
mechi.
Mshambuliaji wa Paris Saint-Germain,
Zlatan Ibrahimovic na kipa wa Bayern Munich, Manuel Neuer wameshika
nafasi ya nne na tano, licha ya kupata pointi sawa na Robben.
Nyota wawili wa Barca, Andres Iniesta
naLuis Suarez - ambao wote wamepewa alama 89 wanakalia nafasi ya sita na
saba, wakati nyota wawili wa Bayern Munich, Bastian Schweinsteiger na Franck Ribery (wote pointi 88) wanashika nafasi ya nane na tisa.
Winga wa Chelsea, Eden Hazard,
waliyepata pointi 88 mwaka jana, ni mchezaji pekee wa ligi kuu England
aliyeingia 10 bora, akiwazidi kete nyota wa Manchester United Robin van
Persie na Radamel Falcao.