HUU NDIO MSIMAMO WA BODI YA LIGI KUHUSIANA NA TFF KUTAKA IPEWE FEDHA ZA KLABU
TFF imeiagiza bodi ya ligi kukata kiasi cha asilimia tano tano kutoka kwenye udhamini wa Vodacom na Azam TV ili ipewe yenyewe.
Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi, Silas Mwakibinga amesema wao ni wawakilishi wa klabu, hivyo wanabaki upande wa klabu.
"Bodi inazaliwa kutoka kwenye ubavu wa klabu, sisi ni wawakilishi wa klabu. Hivyo automatikale tunabaki upande wa klabu," alisema Mwakibinga. Kama bodi hiyo itabaki upande wa klabu hizo 14, maana yake utakuwa umeziokoa kunyongwa fedha zao za udhamini.
Tayari klabu kupitia mwanasheria Dk Damas Ndumbaro zimepinga suala hilo na Mbeya City na Mtibwa Sugar zimetishia kwenda mahakamani.