Published On:Jumapili, 28 Septemba 2014
Posted by Hisia
SAMATTA, ULIMWENGU BAHATI MBAYA, WASHINDA LAKINI MAZEMBE YASHINDWA KWENDA FAINALI
TP Mazembe imefanikiwa kuishinda ES Setif ya Algeria kwa mabao 3-2 katika mechi iliyomalizika hivi punde mjini Lubumbashi.
Lakini
ushindi huo umeshindwa kutosha kwa kuwa Mazembe wanayoichezea
Watanzania Mbwana Samatta na Thomas Ulimwengu haitakwenda fainali ya
Ligi ya Mabingwa Afrika.
Mechi
ya kwanza Setif ilishinda kwa mabao 2-1, hivyo kufungwa 3-2, maana yake
jumla ya mabao 4-4 lakini Setif inapata nafasi ya kwenda fainali
kutokana na idadi ya mabao mawili ya ugenini.
Katika
mechi ya leo, Mazembe ambayo iliwatumia Samatta na baadaye Ulimwengu
ilifanya juhudi kubwa kushinda, lakini mabao mawili yakawatibulia.
Daniel
Niii, Salif Coulibaly na Jonathan Bolingi ndiyo waliifungia Mazembe
mabao matatu huku Abdemalek Ziaya na Soufiane Younos wakifunga mabao ya
Setif.
Sasa Setif inakutana na timu nyingi ya DR Congo. Vita Club ambayo imeingia fainali baada ya kuwatoa Watunisia.