Published On:Jumanne, 30 Septemba 2014
Posted by Hisia
HAWA NDIO WACHEZAJI 26 WALIOITWA TAIFA STARS KUIVAA BENIN
Mbwana Samatta (kushoto) na Thomas Ulimwengu (kulia) wameitwa Taifa Stars
Na Boniface Wambura, Dar es salaam
Wachezaji
26 wameitwa kwenye kikosi cha timu ya Taifa (Taifa Stars) kwa ajili
mechi ya Kalenda ya Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA)
dhidi ya Benin itakayochezwa Oktoba 12 mwaka huu jijini Dar es Salaam.
Kocha
Mart Nooij ambaye yuko Cairo, Misri kwenye kongamano la makocha la
Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF), amesema kikosi cha Taifa
Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager kitaingia kambini
Oktoba 6 mwaka huu jijini Dar es Salaam.
Wachezaji walioitwa ni makipa Deogratias Munishi (Yanga), Aishi Manula (Azam), na Mwadini Ali (Azam).
Mabeki
ni Said Moradi (Azam), Shomari Kapombe (Azam), Oscar Joshua (Yanga),
Nadir Haroub (Yanga), Kelvin Yondani (Yanga), Aggrey Morris (Azam),
Miraji Adam (Simba), Charles Edward (Yanga) na Emmanuel Simwanda
(African Lyon).
Viungo
ni Erasto Nyoni (Azam), Mwinyi Kazimoto (Al Markhiya, Qatar), Amri
Kiemba (Simba), Himid Mao (Azam), Salum Abubakar (Azam), Said Ndemla
(Simba) na Haruna Chanongo (Simba).
Washambuliaji
ni Khamis Mcha (Azam), Simon Msuva (Yanga), Thomas Ulimwengu (TP
Mazembe, DR Congo), Mbwana Samata (TP Mazembe, DR Congo), Mrisho Ngasa
(Yanga), Mwegane Yeya (Mbeya City), na Juma Liuzio (Zesco, Zambia).