Published On:Alhamisi, 25 Septemba 2014
Posted by Hisia
MKATABA WA MOSOTI, SIMBA UMEVUNJWA – FIFA
Mshambuliaji wa Timu ya Yanga, Mrisho Ngassa (17), akimpiga chenga aliyekuwa beki wa Simba, Mkenya, Donald Mtosi wakati mchezo wao wa Nani Mtani Jembe mwezi Desemba mwaka jana
Na Bertha Lumala, Dar es Salaam
Wakati uongozi wa Simba ukidai kuwa bado una mkataba na beki Mkenya Donald Mosoti, Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa) limeitaka klabu hiyo kumlipa fidia beki kwa kuwa mkataba wake umevunjwa.
Katibu Mkuu wa Simba, Stephen Ally alikaririwa na baadhi ya vyombo vya habari nchini jana akisema kuwa Mosoti bado ni mchezaji wao halali kwa vile mkataba kati yao na mchezaji huyo badi haujavunjwa.
Donaldi Mosoti akiwa kazini enzi zake Simba sc
Klabu hiyo kongwe nchini, iliamua kumwacha beki huyo dakika za mwisho za usajili msimu huu ili kumsajili Emmanuel Okwi aliyevunja mkataba wake na Yanga huku mwanasheria wa Mosoti, Felix Majani akidai kuwa uamuzi huo ulifanywa bila kumshirikisha mteja wake.(P.T)
Mwanasheria
huyo anayeishi Ureno amekaririwa na mtandao wa Futaa.com wa Kenya leo
asubuhi akieleza kuwa ilibidi kuvunja mkataba wa Mosoti na Simba kwanza
kabla ya kulifikisha mbele ya FIFA kwa kuwa Simba walikuwa bado wanadai
kwamba Mosoti ni mchezaji wao na walitaka aidha wamuuze au kumtoa kwa
mkopo.
Majani
amesema kuwa mteja wake anataka Simba imlipe fidia kwa kuvunja mkataba
wake ilhali alikuwa bado ana muda wa mwaka mmoja na miezi mitatu
kuitimkia klabu hiyo ya Msimbazi. “Kimsingi Mosoti anataka fidia na
ameomba adhabu za kisoka zichukuliwe dhidi ya Simba, kwa kufungiwa
kusajili wachezaji kwa misimu miwili ijayo ya usajili na tayari FIFA
imeshauandikia barua uongozi wa Simba kuukumbusha juu ya kesi hii,”
amesema Majani.
Beki wa
kushoto Mkenya John Njoroge alikumbana na tatizo kama la Mosoti dhidi ya
Yanga 2011 baada ya klabu hiyo ya Jangwani kuvunja mkataba bila
kumshirikisha na baadaye mchezaji huyo alinufaika kwa kupata fidia ya
Sh. milioni moja za Kenya.
Chanzo:Shaffihdauda