Headlines
Published On:Alhamisi, 25 Septemba 2014
Posted by Hisia

NYAMLANI MGENI RASMI UFUNGUZI WA DR MWAKA SPORTS XTRA NDONDO CUP KESHO!

Jumanne Athuman Nyamlani (kushoto) akiongea na waandishi wa habari kwenye moja ya mikutano yake siku za nyuma

MICHUANO ya Dr Mwaka SPORTS XTRA NDONDO CUP inatarajia kufunguliwa kesho (septemba 26 mwaka huu) kwa mechi ya ufunguzi baina ya Friend’s Rangers na Kiluvya United.
Mechi hiyo kali itapigwa  uwanja wa Makulumla, Magomeni, Dar es salaam kuanzia majira ya saa 10:15 jioni.
Mgeni rasmi katika mechi hiyo atakuwa Mjumbe wa kamati ya Rufaa ya Shirikisho la soka Afrika, CAF na makamu wa Rais wa zamani wa TFF, Jumanne Athuman Nyamlani.
Michuano hii itakayoendeshwa kwa mfumo wa kisasa kabisa itashirikisha wachezaji wa mchangani kutoka timu 32.
Mbali na dimba la Makulumla, viwanja vingine vitakavyotumika katika mashindano hayo ni Kinesi (Shekilango), Benjamini Mkapa (Ilala) na Mizinga (Kigamboni).
 
Mdhamini Mkuu wa michuano ya  Dr Mwaka Sports Extra Ndondo Cup ,Dr Juma Mwaka akifafanua jambo mbele ya wanahabari kuhusiana na michuano hiyo inayotarajiwa kuanza kutimua vumbi kesho Ijumaa kwenye Uwanja wa Makurumla, Magomeni jijini Dar es Salaam.

Timu 32 zitakazoshiriki zimepangwa katika makundi nane yenye timu nne.

Kundi A: Boom fc, Beira Hotspurs, Tabata fc na Tuamoyo
Kund B: Sifa Politani, Vijana Ilala, Kijichi, Micco Villa
Kundi C: Friend’s Rangers, Temeke Market, Kiluvya United na Muheza fc
Kundi D: Ukonga United, Sinza Stars, Congo Shooting na Snow White
Kundi E: Zakhem, Black Six, TP Same na Makumba
Kundi F: Villa Squad, Scud fc, Nyota Afrika na Burudani fc
Kundi H: Stakishari fc, Abajalo, Shelaton na Kimara United

Kundi G: Temeke United, Sifa United, Forteagle na Segerea fc.

About the Author

Posted by Hisia on 9/25/2014 06:55:00 PM. Filed under . You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0. Feel free to leave a response

By Hisia on 9/25/2014 06:55:00 PM. Filed under . Follow any responses to the RSS 2.0. Leave a response

0 comments for "NYAMLANI MGENI RASMI UFUNGUZI WA DR MWAKA SPORTS XTRA NDONDO CUP KESHO!"

Leave a reply

    Blog Archive