Published On:Jumapili, 28 Septemba 2014
Posted by Hisia
RUUD GULLIT AMTOLEA UVIVU VAN GAAL, AMUAMBIA "UMEBORONGA USAJILI, HUIJUI S9OKA YA UINGEREZA"
MWANASOKA
wa zamani wa kimataifa wa Uholanzi, Ruud Gullit ameanzisha vita
ya maneno na kocha Louis van Gaal akibeza usajili wake aliofanya
Manchester United, kwa kusema kwamba umeonyesha kwamba haijui Ligi Kuu
ya England kwa kujaza washambuliaji.
Kocha
huyo wa zamani wa Chelsea na Mwanasoka Bora wa Mwaka Ulaya, awali
alikuwa anamuunga mkono van Gaal, hususan wakati wa Kombe la Dunia
alipotetea mbinu zake katika timu ya taifa ya Uholanzi wakati van Gaal
alipokuwa akikandiwa na magwiji kama Johan Cruyff.
Lakini
Gullit hajafurahishwa na usajili alioufanya Van Gaal Manchester United,
akisaini wachezaji kama Angel Di Maria, Radamel Falcao, Ander Herrera,
Luke Shaw, Daley Blind na Marcos Rojo wote wakigharimu Pauni Milioni
170, huku akipuuza kusajili mabeki.
Ruud Gullit amesema Van Gaal amefanya makos a kusajili washambuliaji zaidi kuliko mabaki
Na
mchezaji huyo wa zamani wa AC Milan anafikiri kwamba van Gaal ameweka
imani kubwa kwa safu ya ushambuliaji ambayo ni utamaduni wa Kiholanzi,
na akashindwa kuielewa Ligi Kuu ya England.
Gullit
amesema: "Inawezekanaje katika dunia hii kocha mzoefu na mwenye
mafanikio anaweza kuanza msimu Man United bila kununua mabeki kadhaa
halisi? Bado nastaajabishwa na usajili na uhamisho wake. Kama utaimarisha safu ya kiungo na ushambuliaji pekee kisha ukadharau nguvu ya timu nyingine za Ligi Kuu.
Kama unataka
kufurukuta katika mashindano makubwa kwenye soka ya England uanze na
kujenga msingi na kisha baadaye ujenge paa la nyumba yako. Van Gaal
amefanya kinyume ya hivi.