Published On:Jumatano, 24 Septemba 2014
Posted by Hisia
KOCHA COASTAL UNION AWACHANA 'LAIVU' WAANDISHI WA MICHEZO BONGO
Na Mwandishi Wetu, Tanga
KOCHA
Mkuu wa Coastal Union, Yusuph Chippo amewataka waandishi wa habari
za michezo hapa nchini kuacha kupika stori kwenye vyombo vya habari
badala yake waandika habari zilizokuwa na ukweli.
Hatua hiyo ya Kocha Chippo inatokana na taarifa iliyoandikwa
kwenye gazeti
moja la michezo hapa nchini likimnukuu kocha huyo kusema kuwa tatizo
la Simba lipo kwenye beki na watapata wakati mgumu watakapocheza
na timu ambayo inawashambuliaji wenye kasi jambo ambalo hakulisema.
Chippo
alisema kuwa kitendo hicho kimemshangaza sana kuona waandishi wanaacha
kufanya kazi zao kwa ueledi mkubwa kwa lengo la kuchochea kasi
ya maendeleo ya soka nchini badala yake wamekuwa wamekuwa wakitunga
stori ambazo hazipo.
Alisema
kubwa zaidi lililomshangaza ni kuona taarifa hiyo ikiandika kuwa
alisema kwa jinsi Simba inavyocheza itapata wakati mgumu itakapocheza
na Yanga, kiungo na washambuliajio wako vizuri lakini beki
yao ina tatizo hivyo wanahitaji kuangalia kwa umakini hasa washambuliaji
wa kasi.
Aidha
alisema habari hizo hazifahamu wala hakuzungumza na mwandishi wa aina yoyote ile hivyo kuwataka kuacha kufanya hivyo
kwani wanatengeneza
masuala yasiyokuwa mazuri kwenye jamii hususani ya wanamichezo
hapa nchini.
“Tunafahamu kuwa waandishi wa habari wanakazi kubwa sana ya
kuielimisha
jamii inayowazunguka hivyo nawasihi fanyeni kazi zetu kwa ueledi
mkubwa na kuacha kupika stori kwenye vyombo vyenu “Alisema Chippo.
Hata
hiyo alisema timu hiyo imeanza kuipiga mahesabu ya kuhakikisha inachukua
pointi tatu muhimu dhidi ya Mbeya City kwenye mechi ya Ligi kuu
soka Tanzania bara itakayochezwa Jumamosi wiki hii kwenye uwanja wa
Sokoine Mbeya.
Chippo
alisema kuwa kikosi chake kimekuwa na hari mpya hivyo
atahakikisha
anawaanda vizuri wachezaji wake ili waweze kucheza
kandanda
nzuri ambalo linawawezesha kupata mabao mengi kwenye mechi hiyo.
Coastal
Union tayari imekwisha kuwasili mkoani Mbeya ikijiandaa na mechi
yake dhidi ya Mbeya City itakayochezwa kwenye uwanja wa sokoine mkoani humo