Headlines
Published On:Jumanne, 23 Septemba 2014
Posted by Hisia

HUYU NDIO MCHEZAJI ALIYEUUMIA ZAIDI YA WOTE BAADA YA FERGUSON KUTUNDIKA MIKOBA YA UKOCHA MAN UNITED.



Robin van Persie (kulia) alihuzunika sana baada ya kupata taarifa za kustaafu kwa  Sir Alex Ferguson

MAAMUZI ya Sir Alex Ferguson kustaafu kazi ya ukocha Old Trafford yalishitua kikosi kizima cha Manchester United, lakini hakuna aliyechukulia habari hizo kwa uzito wa juu kuliko Robin va Persie.
Hayo ni maoni ya Rio Ferdinand ambaye amefichua siri hiyo akidai kuwa RVP alihangaika sana kuzoea hali hiyo.
Ferguson alikuwa sababu kubwa ya Van Persie kujiunga na Man United akitokea Arsenal kwa ada ya uhamisho ya paundi milioni 24 mwaka 2012.
Van Persie alongside Radamel Falcao during the dismal 5-3 defeat away at Leicester City on Sunday 
Van Persie akiwa na Radamel Falcao katika kipigo cha 5-3 siku ya jumapili dhidi ya Leicester City  
Rio Ferdinand - who moved to Queens Park Rangers in the summer - was talking to MUTV
Rio Ferdinand - aliyejiunga na Queens Park Rangers  majira ya kiangazi mwaka huu-alikuwa anazungumza na MUTV

Magoli 31 ya RVP katika msimu wake wa kwanza Man United yaliwasaidia mashetani wekundu kutwaa ubingwa wa ligi kuu wakiwapora Man City. 
Ferdinand aliwaambia MUTV: "Taarifa ilikuwa mbaya kwa kila mtu, lakini mtu ambaye aliumia sana kuliko yeyote ni Robin. Alijiunga mwaka mmoja kabla, alionja mafanikio na alihitaji zaidi.
"Kiukweli unaweza kuona yeye ndiye aliyeumia sana kuliko mwingine yeyote kwa muda ule".
Van Persie alihangaika katika utawala wa David Moyes msimu uliofuata na sasa yuko chini ya Mholanzi mwenzake, Lousi Van Gaal.

About the Author

Posted by Hisia on 9/23/2014 08:49:00 AM. Filed under . You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0. Feel free to leave a response

By Hisia on 9/23/2014 08:49:00 AM. Filed under . Follow any responses to the RSS 2.0. Leave a response

0 comments for "HUYU NDIO MCHEZAJI ALIYEUUMIA ZAIDI YA WOTE BAADA YA FERGUSON KUTUNDIKA MIKOBA YA UKOCHA MAN UNITED. "

Leave a reply

    Blog Archive