Published On:Alhamisi, 25 Septemba 2014
Posted by Hisia
MAJAGOO WA JIJI LIVERPOOL WAKALIA KITI CHA MOTO UEFA.
UEFA inajiandaa kuichunguza Liverpool kwa kudaiwa kuvunja sheria ya FFP
LIVERPOOL wanachunguzwa na UEFA kwa kudaiwa kuvunja sheria ya matumizi ya fedha.
Liverpool, Monaco, Inter Milan na Roma —
ambao hawakuwepo katika michuano ya Ulaya msimu uliopita wametuma
akaunti zao UEFA na sasa wanasubiri kuulizwa juu ya taarifa nyingine za
kifedha.
Hakuna vikwazo watakavyowekewa kwa hatua hii, ingawa kifungo cha kutopata fedha za ligi ya mabingwa kinaweza kufuata.