Published On:Ijumaa, 26 Septemba 2014
Posted by Hisia
FIFA YAPIGA STOP MAGUMASHI YA UMILIKI WA TATU KWA MCHEZAJI...KIKOSI KAZI CHAUNDWA KUUNDA SHERIA MPYA
KAMATI
Kuu ya Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA) imepiga jura
kuzuia umbilici wa tatu wa wachezaji ambao umekuwa ukiruhusu wawekezaji
wa nje kunufaika na uhamisho.
Rais wa FIFA, Sepp Blatter amesema kikosi kazi kitaandika sheri a sasa ya kufuata.
Uamuzi
huo wa leo ni ushindi wa kisiasa kwa Shirikisho la Soka Ulaya (UEFA) na
Rais wake, Michel Platini, ambaye amekuwa akirudia kuitaka FIFA
kuchukua hatua.
Usajili
wa Manchester City wa Pauni Milioni 32 kwa Eliaquim Mangala kutoka
Porto msimu huu ni moja ya mifano ya dili za umiliki wa pande tatu
Usajili wa Manchester United pia kwa beki Marcos Rojo uliripotiwa kuhusisha panda tatu za wamiliki
Umiliki
wa panda tatu ni maarufu mawakala, wawekezaji na klabu Latin Amerika,
Hispania na Ureno, lakini tayari umezuiwa nchini England.
Licha
ya hivyo, klabu kadhaa za Ligi Kuu England zimeripotiwa kununua
wachezaji kwa wamiliki wa tatu pia ili kufanikisha nyota zilizowasajili
msimu huu.
Eliquim
Mangala aliyenunuliwa kwa Pauni Milioni 32 kutoka Porto kwenda
Manchester City, Marcos Rojo Pauni Milioni 16 kutoka Sporting Lisbon
kwenda Manchester United na Lazar Markovic Pauni Milioni 20 kutoka
Benfica kwenda Liverpool wote waliripotiwa kununuliwa kwa wamiliki
watatu.
UEFA inasema
uhamisho wa aina hiyo unazigharimu klabu fedha nyingi wakati wa kununua
wachezaji na wakati mwingine unawakwamisha wachezaji wanapotaka
kununuliwa na klabu ambazo haziko tayari kulipa kwa wamiliki watatu- na
haina msaada kwa mchezaji ambaye anaachwa na klabu.