Published On:Jumatatu, 29 Septemba 2014
Posted by Hisia
Phiri awabadilikia Okwi, Tambwe Simba
Kocha Mkuu wa Simba, Mzambia, Patrick Phiri.
KOCHA Mkuu wa Simba, Mzambia, Patrick Phiri, ametamka kuwa, hafurahishwi na safu yake ya ushambuliaji inayoongozwa na Mganda, Emmanuel Okwi na Mrundi, Amissi Tambwe.
Kauli hiyo ameitoa mara baada ya kumalizika kwa mechi ya Ligi Kuu
Bara dhidi ya Polisi Morogoro iliyochezwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini
Dar es Salaam na matokeo kumalizika kwa sare ya bao 1-1.
Timu hiyo, hadi hivi sasa imefanikiwa kufunga mabao matatu ikiwa imecheza michezo miwili pekee ya ligi dhidi ya Coastal Union (2-2) na Polisi Morogoro (1-1).
Timu hiyo, hadi hivi sasa imefanikiwa kufunga mabao matatu ikiwa imecheza michezo miwili pekee ya ligi dhidi ya Coastal Union (2-2) na Polisi Morogoro (1-1).
Akizungumza na Championi Jumatatu, Phiri alisema kuwa kwanza
anaipongeza safu ya kiungo inayoongozwa na Jonas Mkude na Pierre Kwizera
kwa kutimiza majukumu vizuri kwa kuwatengenezea mipira mizuri ya
kufunga mabao.
Phiri alisema safu yake hiyo ya ushambuliaji inakosa nafasi nyingi za wazi za kufunga mabao.
Aliongeza kuwa, washambuliaji hao wanahitaji kubadilika kwa haraka kwa kuhakikisha wanafunga mabao kwa kila nafasi watakayoipata ili timu ipate ushindi katika mechi zake.
Aliongeza kuwa, washambuliaji hao wanahitaji kubadilika kwa haraka kwa kuhakikisha wanafunga mabao kwa kila nafasi watakayoipata ili timu ipate ushindi katika mechi zake.
“Mwanzoni nilikuwa na tatizo la kiungo kabla ya kurejea uwanjani
Mkude akitoka kwenye majeraha, tatizo nililoliona kwenye mechi ya kwanza
ya ligi dhidi ya Coastal Union.
“Tatizo hilo nikalimaliza kwa kumpanga Mkude kwenye mechi ya Polisi
Morogoro, hivi sasa tatizo limehamia kwenye safu ya ushambuliaji
inayochezwa na Okwi na Tambwe ambao wanashindwa kutumia nafasi nyingi za
kufunga mabao.
“Ninataka kila mchezaji atimize majukumu yake vizuri kwa mabeki
kuokoa hatari, viungo kuchezesha timu na washambuliaji kufunga,” alisema
Phiri.