TIMU
ya AS Vita ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) imekata tiketi ya
kucheza Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika, hiyo ikiwa ni mara ya kwanza
tangu mwaka 1981 baada ya jana kuifunga CS Sfaxien mabao 2-1 katika
Nusu Fainali ya pili.
Vigogo
hao Kinshasa wanasonga mbele katika fainali itakayopigwa Oktoba kwa
ushindi wa jumla wa 4-2, baada ya awali kuifunga Sfax kama jana katika
mchezo wa kwanza mjini Kinshasa.
Mabingwa
hao wa mwaka 1973 sasa wanasubiri mshindi wa jumla wa Nusu Fainali
nyingine ya pili leo mjini Lubumbashi kati ya wenyeji TP Mazembe na ES
Setif ya Algeria. Mazembe walifungwa 2-1 katika mchezo wa kwanza na leo
wanahtaji ushindi wa 1-0 kuungana na Vita fainali.
About the Author
Posted by Hisia
on 9/28/2014 05:14:00 PM. Filed under
Afrikaligi
.
You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0.
Feel free to leave a response
By Hisia
on 9/28/2014 05:14:00 PM. Filed under
Afrikaligi
.
Follow any responses to the RSS 2.0. Leave a response