Headlines
Published On:Alhamisi, 25 Septemba 2014
Posted by Hisia

RAUNDI YA NNE CAPITAL ONE: CHELSEA WAPANGWA NA 'VIBONDE', MAN CITY v NEWCASTLE, LIVERPOOL KUUTAFUNA MFUPA WA SWANSEA!

Frank Lampard akishangilia goli lake la tatu katika mechi mbili dhidi ya  Sheffield jana
SHREWSBURY Town, timu pekee ya daraja la chini zaidi iliyosalia katika michuano ya kombe la ligi 'Capital One Cup' amepangwa kukutana na timu ngumu ya ligi kuu ya England, Chelsea kwenye mechi ya raundi ya nne.
 Raundi iliyopita Shrews inayocheza daraja la pili iliwaondoa mabingwa wa Championship, Norwich na  sasa itawakaribisha Chelsea walioshinda 2-1 dhidi ya Bolton jana usiku.
Mabingwa watetezi, Manchester City, walioitoa Sheffield jana kwa kuifunga mabao 7-0  katika dimba la Etihad watachuana na Newcastle inayocheza ligi kuu.
Liverpool waliosonga mbele kwa penati 14-13 dhidi ya Middlesbrough jumanne usiku, watachuana na Swansea City, zote zinacheza ligi kuu.
Stoke wataikaribisha Southampton , wakati Tottenham watakuwa nyumbani dhidi ya  Brighton.
Mechi nyingine za raundi ya nne zitawakutanisha  Sheffield United watakaosafiri kuifuata MK Dons na Fulham watakabiliana na Derby.

Capital One Cup: MECHI ZA RAUNDI YA NNE

Tottenham Hotspur vs Brighton
Stoke vs Southampton
Bournemouth vs West Brom
Shrewsbury vs Chelsea
Liverpool vs Swansea
MK Dons vs Sheffield United
Manchester City vs Newcastle United
Ties to be played on the week commencing 27 October 2014 
Liverpool's Suso (right) celebrates his goal before the penalty shootout win over Middlesbrough
Suso wa Liverpool (kulia) akishangilia goli lake la penalti dhidi ya Middlesbrough

About the Author

Posted by Hisia on 9/25/2014 06:58:00 PM. Filed under . You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0. Feel free to leave a response

By Hisia on 9/25/2014 06:58:00 PM. Filed under . Follow any responses to the RSS 2.0. Leave a response

0 comments for "RAUNDI YA NNE CAPITAL ONE: CHELSEA WAPANGWA NA 'VIBONDE', MAN CITY v NEWCASTLE, LIVERPOOL KUUTAFUNA MFUPA WA SWANSEA!"

Leave a reply

    Blog Archive