Published On:Ijumaa, 26 Septemba 2014
Posted by Hisia
WENGER AWAANZISHIA TENA MAN CITY NA USAJILI WAO WA KIMAGUMASHI KWA FRANK LAMPARD
MPANGO
wowote wa kuongeza muda wa Frank Lampard kuendelea kucheza kwa
Manchester City unaweza kuibua maswali zaidi ya kimaadili juu ya
uhamisho wake, kwa mujibu wa kocha Arsenal, Arsene Wenger.
Lampard
alisaini timu ya Ligi Kuu ya Marekani (MLS), New York City baada ya
kutemwa Chelsea, kabla ya kurejea ghafla Ligi Kuu ya England kujiunga na
mabingwa, ambao pamoja na kuinunua timu ya baseball ya wakanunua na
hisa timu hiyo ya MLS.
Kiwango
kizuri cha mkongwe huyo mwenye umri wa miaka 36, aliyefunga mabao
mawili katika ushindi wa 7-0 Kombe la Ligi, maarufu kama Capital One Cup
dhidi ya Sheffield Jumatano, umeibua tetesi kwamba City itaangalia
uwezekano wa kumbakiza ifikapo Januari.
Msimu
wa MLS 2015 unatarajiwa kuanza tena Machi, na Lampard amesema hajafanya
majadiliano coyote na City juu ya mustakabali wake mwishoni mwa mwaka.
Wenger,
ambaye alimrudisha kwa mkopo Nahodha wake wa zamani The Gunners,
Thierry Henry kutoka New York Red Bulls Januari 2012, anaamini namna
coyote ya kuongeza mkataba wa mkopo wa Lampard kwa sasa haitakuwa nzuri,
hata ikiwa ni ndani ya utaratibu wa Ligi Kuu.
"Wakati wote una maamuzi ya aina mbili, moja ya kimaadili na pili na ya kisheria na ni juu ya unavyochukulia,"amesema Wenger.
"Nafikiri, hii ni sheria? lazima uheshimu hilo na kisha mchezaji lazima atazame uamuzi wake. Naheshimu ukweli kwamba anataka kucheza katika kiwango cha juu na labda hakuwa na nafasi zaidi Chelsea. Sijui haswa kilicho nyuma ya hili,".
"Ulikuwa ni mpango wake kwenda New York na kwenda Man City? Sina uhakika. Nafikiri kabisa alitaka kwenda nje na kutua New York, na (kisha) kupewa ofa ya kurudi Ligi Kuu England na kuichukua. Anaweza kufafanua vizuri yeye mwenyewe kuliko ninavyofanya, sijui nini kipo nyuma ya hili,"amesema Wenger.