Headlines
Published On:Jumamosi, 27 Septemba 2014
Posted by Hisia

AZAMU YAFANYA KWELI YAIBAMIZA RUVU GOLI 2 - 0, KAVUMBANGU APIGA GOLI ZOTE MBILI - CHAMAZI

AZAM FC imekaa kileleni mwa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara baada ya kuichapa mabao 2-0 Ruvu Shooting ya Pwani mabao 2-0 Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam. Azam FC walikwenda kupumzika wakiwa wanaongoza bao 1-0 lililofungwa na Mrundi, Didier Kavumbangu, ambalo hilo linakuwa bao lake la tatu msimu baada ya kufunga mawili katika ushindi wa 3-0 kwenye mchezo wa kwanza dhidi ya Polisi Moro. Kavumbangu alifunga bao hilo dakika ya 40, baada ya kuuwahi mpira uliopanguliwa na kipa wa Ruvu, Abdallah Abdallah kufutia shuti la Kipre Tchetche aliyeungaisha krosi maridadi ya Shomary Kapombe.
Kavumbangu akipongezwa na wenzake leo Chamazi
Kavumbangu akimtoka Salvatory Ntebe wa Ruvu Shooting

Kipindi cha pili, kocha Mcameroon, Joseph Marius Omog alianza na mabadiliko akimpumzisha beki Kapombe aliyeumia na nafasi yake ikichukuliwa na Erasto Nyoni.  Kavumbagu aliwainua vitini tena mashabiki wa timu ya Alhaj Sheikh Said Salim Awadh Bakhresa dakika ya 50 baada ya kufunga bao la pili kwa kichwa akimalizia krosi ya Himi Mao Mkami. Salum Abubakar ‘ Sure Boy’ aliinyima Azam FC bao la tatu baada ya kushindwa kuunganisha krosi nzuri ya Kavumbangu dakika ya 70. Dakika ya 75, Kavumbangu alipata nafasi nzuri ya kufunga hat trick ya kwanza Ligi Kuu msimu huu baada ya kutengewa pasi nzuri na Kipre Tchetche, lakini akashindwa kuumiliki vizuri mpira ukaokolewa na mabeki. Kikosi cha Azam FC kilikuwa; Aishi Manula, Shomary Kapombe/Erasto Nyoni dk46, Gadiel Michael, David Mwantika/Said Mourad dk68, Aggrey Morris, Kipre Balou, Himid Mao/Farid Mussa dk83, Mudathir Yahya, Didier Kavumbangu, Salum Abubakar ‘Sure Boy’ na Kipee Tchetche.   Ruvu Shooting; Abdallah Abdallah, Said Madega, Yussuf Nguya, Salvatory Ntebe, Hamisi Kasanga, Kassim Zabi, Juma Mpakala, Ally Mkanga/Baraka Mtuwo dk64, Justin Chagula, Abdulrahman Abdulrahman na Juma Nade/Ayoub Kitala dk53.

About the Author

Posted by Hisia on 9/27/2014 06:46:00 PM. Filed under . You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0. Feel free to leave a response

By Hisia on 9/27/2014 06:46:00 PM. Filed under . Follow any responses to the RSS 2.0. Leave a response

0 comments for "AZAMU YAFANYA KWELI YAIBAMIZA RUVU GOLI 2 - 0, KAVUMBANGU APIGA GOLI ZOTE MBILI - CHAMAZI"

Leave a reply

    Blog Archive