Published On:Jumamosi, 27 Septemba 2014
Posted by Hisia
COASTAL UNION YAIPA USHAURI TFF KUHUSU VITENDO VYA KISHIRIKINA UWANJANI
Na Mwandishi Wetu, Mbeya
KLABU ya Coastal Union imelishauri Shirikisho la soka nchini (TFF)
kuhakikisha wanakuwa wakali kwenye kidhibiti vitendo vya kishirikina vinavyojitokeza
kabla ya kuanza michezo ya Ligi kuu soka Tanzania bara kwani hali hiyo
inadumaza maendeleo ya soka nchini.
Hali hiyo isipodhibitiwa upo uwezekano mkubwa wa timu za
Tanzania kushindwa kufanya vizuri kwenye mashindano makubwa wanayocheza nje za
nchi.
Kauli hiyo imetolewa leo na Mjumbe wa Kamati ya Utendaji wa
Coastal Union, Albert Peter mara baada ya usiku wa jana saa saba usiku
mashabiki ambao inasadikika ni wa timu ya Mbeya City kumwaga madawa kwenye
kambi ya Coastal Union jambo ambalo sio zuri.
Amesema iwekwe sheria kali kwa timu itakayobainika kufanya
ili kutokomeza vitendo hivyo.
Licha ya hayo amesema kikosi cha timu hiyo kimejipanga vizuri ili kuweza kuhakikisha kinafanya vizuri kwenye michezo yao ya Ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara ili kuweza kuchukua ubingwa wa Ligi hiyo.