Headlines
Published On:Jumatano, 24 Septemba 2014
Posted by Hisia

ARSENAL YATUPWA NJE CAPITAL ONE NA SOUTHAMTPON

ARSENAL imefungwa mabao 2-1 na Southamtpon katika Kombe la Ligi, maarufu kama Capital One Cup usiku wa kuamkia leo Uwanja wa Emirates.    Alexis Sanchez alitangulia kuwafungia Gunners  dakika ya 14 kwa mpira wa adhabu, kabla ya Dusan Tadic kusawazisha dakika sita baadaye kwa penalty, kufuatia Tomas Rosicky kumchezea rafu Sadio Mane. 
Mshindi wa mechi; Nathaniel Clyne akiifungia Southampton bao la ushindi jana
Nathaniel Clyne akaifungia Southampton bao la ushindi kwa shuti la umbali wa mita 30 dakika ya 40 katika mchezo ambao kiungo anayetoka kwenye majeruhi wa Arsenal, Abou Diaby alianza kwenye kikosi cha kwanza kwa mara ya kwanza tangu Machi 2013.  
Kikosi cha Arsenal kilikuwa: Ospina, Bellerin/Akpom dk86, Chambers, Hayden, Coquelin, Rosicky, Diaby/Cazorla dk67, Campbell/Oxlade-Chamberlain dk71, Wilshere, Podolski na Sanchez.   
Southampton: Forster, Clyne, Fonte, Gardos, Targett/Bertrand, Wanyama, Schneiderlin, Mane/Long dk72, Davis, Tadic na Pelle.
Jack Wilshere passes the ball away from a Sadio Mane tackle. The England star was part of a strong attacking line-up fielded by Arsene Wenger 
Jack Wilshere akijaribu kuondosha mpira mbali ya Sadio Mane katika mchezo wa usiku wa kuamkia leo.

About the Author

Posted by Hisia on 9/24/2014 06:35:00 AM. Filed under . You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0. Feel free to leave a response

By Hisia on 9/24/2014 06:35:00 AM. Filed under . Follow any responses to the RSS 2.0. Leave a response

0 comments for "ARSENAL YATUPWA NJE CAPITAL ONE NA SOUTHAMTPON "

Leave a reply

    Blog Archive