Published On:Jumatatu, 22 Septemba 2014
Posted by Hisia
Video: Lampard Asema Kilichomzuia Kushangilia Bao La Kuiokoa Man City
Kiungo kutoka nchini Uingereza Frank Lampard ametoa sababu
ya kwa nini alishindwa kushangilia mara baada ya kuiwezesha klabu ya Man
City kupata bao la kusawazisha wakati wa mchezo wa ligi kuu dhidi ya
Chelsea hapo jana.
Lampard, amesema ilikuwa ni vugumu kwake kushangilia bao alilofunga
kutokana na mapenzi ya dhati aliyo nayo dhidi ya klabu ya Chelsea ambayo
ilimtunza kwa miaka 13 iliyopita akitokea West Ham utd.
Lampard, amesema bado anaipenda klabu hiyo na siku zote anahisi ni
sehemu ya maisha yake hivyo hawezi kuiumiza nafsi yake kutokana na
mazingira aliopo sasa ambayo ni tofauti na klabu hiyo ya magharibi mwa
London.
Amesema ni vizuri kwake kufanya kazi kwa uadilifu na anatambua
uweledi uliopo kutokana na uwajibikaji wake anapokuwa uwanjani hususan
inapotokea anacheza dhidi ya klabu anayoipenda.
“Naamini sijakosea na wala sijamkwaza yoyote, nimetimiza wajibu wangu
ndani ya uwanja na suala la kushangilia ama kutoshangilia lilikuwa
ndani ya maamuzi yangu hivyo ni jambo la kawaida.” Amesema Lampard
Lampard, anaitumikiwa klabu ya Man city kwa mkopo akitokea nchini
Marekani ambapo alisajiliwa na klabu ya New York City FC miezi miwiwli
iliyopita baada ya kumaliza mkataba na klabu ya Chelsea.
Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 36 aliondoka Chelsea huku akiwa
ameweka rekodi ya kuwa mfungaji bora kwa wakati wote wa klabu hiyo baada
ya kufunga mabao 211 katika michezo 648 aliyocheza akiwa Stamford
Bridge.