MABINGWA
watetezi wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara leo wameanza vyema mbio
za kubakiza taji lao, baada ya kuichapa Polisi Morogoro mabao 3-1 Uwanja
wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam.
Ushindi
huo unaomfuta machozi kocha Mcameroon, Joseph Marius Omog baada ya
kufungwa 3-0 na Yanga SC katika mchezo wa Ngao ya Jamii ulitokana na
mabao ya Didier Kvumbangu mawili na Aggrey Morris.
Azam
walikwenda kupumzika wakiwa wanaongoza mabao 2-0, Kavumbangu akianza
kufunga dakika ya 14 akiunganisha pasi ya Kipre Tchetche katikati ya
beki na kipa wa Polisi.
|
Shujaa; Didier Kavumbangu akishangilia baada ya kuifungia Azam FC mabao mawili katika ushindi wa 3-1 |
|
Didier Kavumbangu akimtoka beki wa Polisi leo Uwanja wa Azam Complex, Chamazi |
Beki
Aggrey Morris akaipatia bao la pili Azam FC dakika ya 23 aliyemalizia
mpira wa adhabu uliopigwa na Kipre Tchetche kufuatia beki Gardiel
Michael kuchezewa rafu na Bantu Admin.
Baada
ya mabao hayo mawili ya haraka haraka, kocha wa Polisi Morogoro,
Mohammed Adolph ‘Rishard’ alimpumzisha kiungo Bantu Admin na kumuingiza
James Mganda.
Mabadiliko
hayo kidogo yaliituliza Polisi na kuanza kufika kwenye lango la Azam,
ingawa hawakufanikiwa kupata bao hadi dakika 45 za kwanza
zilipokamilika.
Mshambuliaji wa zamani wa Simba SC, Danny Mrwanda alidhibitiwa vikali na mabeki wa Azam leo.
Kipindi
cha pili, Azam FC ilirudi vizuri na kusukuma mashambulizi mfululizo
langoni mwa Polisi, lakini mshambuliaji Kipre Tchetche alikosa mabao
matatu ya wazi.
Nahoda
Bakari aliipatia bao Polisi dakika ya 60 baada ya kuanzishiwa kona fupi
na kumtungua kwa shuti la umbali 22 kipa Aishi Manula.
Didier Kavumbangu aliifungia bao la tatu Azam FC dakika ya 90 akimalizia krosi ya Farid Malik.
Kikosi
cha Azam FC kilikuwa; Aishi Manula, Shomary Kapombe, Gardiel Michael,
David Mwantika, Aggrey Morris, Kipre Balou, Himid Mao/Khamis Mcha
‘Vialli’ dk72, Mudathir Yahya, Didier Kavumbangu, Kipre Tchetche/Farid
Malik dk72 na Salum Abubakar.
Polisi
Moro; Tony Kavishe, Rogeri Fred, Simon Fanuel, Ally Feruzi Telu,
Lulanga Mapunda, Said Jella, Bantu Admin/James Mganda dk22, Nahoda
Bakari/Suleiman Kassim ‘Selembe’ dk65, Danny Mrwanda, Machaku Salum na
Nicholas Kabipe/Edgar Charles dk65.
About the Author
Posted by Hisia
on 9/20/2014 07:02:00 PM. Filed under
Vpl
.
You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0.
Feel free to leave a response
By Hisia
on 9/20/2014 07:02:00 PM. Filed under
Vpl
.
Follow any responses to the RSS 2.0. Leave a response