Published On:Alhamisi, 11 Septemba 2014
Posted by Hisia
CHAMA CHA SOKA CHA MISRI CHAMTETEA KOCHA GHARIB BAADA YA MAFARAO KUTANDIKWA MECHI MBILI KUFUZU AFCON 2015
MWENYEKITI wa chama cha soka cha
Misri, Gamal Allam amemhakikishia kocha mkuu wa timu ya Taifa ya nchi hiyo,
Shawky Gharib kwamba hatafukuzwa.
Mafarao walipoteza mechi ya pili ya
kufuzu AFCON 2015 baada ya kufungwa 10 na Tunisia na kupunguza matumaini ya
kusonga mbele katika safari hiyo ya Morocco.
Misri walifungwa 2-0 katika mechi ya
kwanza ya makundi dhidi ya Senegal.
“Shawky Gharib hataondoka katika
nafasi yake, ataendelea kuwa kocha wa Mafarao,” Allam alisema baada ya mechi.
“Kwasasa siwezi kulizungumzia zaidi
hilo, tutakuwa na kikao naye na benchi zima la ufundi kuzungumzia sababu za
timu kupoteza mechi mbili.”
Mashabiki wa Misri waliohudhuria
mechi hiyo walikitaka chama cha soka nchini humo kumfukuza kazi kocha mkuu.
Misri itacheza mechi nyingine dhidi
ya Botswana mwezi Oktoba mwaka huu.
Mafarao hawajawahi kufuzu AFCON tangu walipotwaa ubingwa mwaka 2010 nchini Angola.