Published On:Ijumaa, 19 Septemba 2014
Posted by Hisia
KATIBU COASTAL UNION KUBURUZWA 'KIZIMBA' CHA MAADILI TFF
Na Boniface Wambura, DAR ES SALAAM
KATIBU
Mkuu wa Coastal Union, Kassim El Siagi atafikishwa kwenye Kamati ya
Maadili ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kwa kushinikiza mkutano wa
wanachama wa klabu hiyo ufanyike bila kuandaliwa na Kamati ya Utendaji.
Pia
El Siagi alitumia vyombo vya habari kuishambulia TFF ambayo haikutambua
uamuzi wa mkutano huo ulioelezwa kumdumaza Makamu Mwenyekiti wa klabu
hiyo Steven Mnguto.
TFF ilimtuma Mkurugenzi wake Msaidizi wa Sheria na Uanachama kufanya uchunguzi wa mgogoro uliokuwa unaendelea katika klabu hiyo.
Baada
ya kupokea taarifa ya uchunguzi huo, TFF imebaini kuwa Mwenyekiti na
Mweka Hazina wa klabu hiyo walishajiuzulu, hivyo uitishwe uchaguzi
haraka na kujaza nafasi hizo na nyingine zilizo wazi.
Pia
wajumbe wa Kamati ya Utendaji ya Coastal Union, Salim Amir na Albert
Peter wameonywa kwa kushiriki katika mkutano ambao wanajua haukuandaliwa
na Kamati ya Utendaji.
Vilevile
uchunguzi wa TFF umebaini kuwa ushiriki wa Salim Bawazir na Akida
Machai kwenye vikao vya Kamati ya Utendaji ya Coastal Union si halali
kwa vile wajumbe wa kamati hiyo wanachaguliwa na Mkutano Mkuu na si
kuteuliwa na Mwenyekiti.
Kwa
vile kutakuwa na uchaguzi wa kujaza nafasi ambazo zipo wazi, uchaguzi
huo utasimamiwa na Kamati ya Uchaguzi ya Coastal Union kwa kushirikiana
na Kamati ya Uchaguzi ya TFF, na Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Tanga
na Coastal Union watafanya uhakiki wa reja ya wanachama.