Published On:Jumamosi, 20 Septemba 2014
Posted by Hisia
SAMATTA NA ULIMWENGU KATIKA MECHI NZITO TP MAZEMBE UGENINI LEO
KLABU
ya Entente Setif ya Algeria insignia kwenye mechi ya kiasi dhidi ya TP
Mazembe katika Nusu Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika leo Uwanja wa
Stade du 8 Mai 1945 usiku wa leo.
Huo
utakuwa mchezo wa pili kuzikutanisha timu hizo mfululizo kwa michuano
ya Afrika, baada ya awali kukutana mwaka jana katika hatua ya makundi ya
Kombe la Shirikisho.
Mazembe haikufungwa na Setif katika Kundi B wakitoa safe ya 1-1 nchini Algeria kabla ya kuwafunga 4-2 mjini Lubumbashi.
Setif
ilishika mkia katika Kundi B wakati Mazembe ilikwenda Nusu Fainali
ambako walitolewa na CS Sfaxien ya Tunisia kwenye fainali kwa kufungwa
1-0 matokeo ya jumla.
“Tutajaribu
kulipa kisasi cha kufungwa 4-2 msimu uliopita, na pia tulikutana nap
katika hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa mwaka 2010,” alisema kocha
wa Setif, Kheireddine Madoui.
Setif
haijafungwa katika Ligi ya Mabingwa msimu huu chini ya kocha mwenye
umri wa miaka 37 na ilitinga Nusu Fainali baada ya sare nne na kushinda
mechi mbili kwenye kundi lake.
Wakati
huo huo, Mazembe haina rekodi ya uhakika ya mechi za ugenini, imefungwa
mara mbili na kutoa sare tatu katika mechi zake tano za ugenini mwaka
huu.
Lakini
kiungo Rainford Kalaba, anaamini wanaweza kushinda mechi yao ya kwanza
ugenini leo tangu Machi, 2013 walipoichapa Centre Chiefs of Botswana
1-0.
"Moyoni
mwangu, naweza kufikiria kitu hicho tu: Kwenda Setif kushinda. Mechi za
Nusu Fainali zina uzito tofauti, kwa sababu zinafungua milango ya
fainali," amesema Kalaba.
Washambuliaji wawili Watanzania, Mbwana Samatta na Thomas Ulimwengu wanatarajiwa kuendelea kuibeba Mazembe leo.
Nusu Fainali nyingine ni kati ya AS Vita ya DRC dhidi ya CX Sfaxien ya Tunisia mjini Kinshasa.
Mbwana Samatta anatarajiwa kuendelea kuibeba Mazembe leo |