Published On:Jumamosi, 13 Septemba 2014
Posted by Hisia
SIMBA KWANZA, NDANDA FC BAADAYE'..RAIS WA SIMBA EVANS AVEVA MOTO WA KUOTEA MBALI - HAYO NDIO MANENO YA WANAMTWARA
Wanachama na mashabiki wa Simba
Sports Club wakiwa katika picha na Rais wao, Evans Elieza Aveva
(aliyevalishwa shada la ua) katika uzinduzi wa tawi la klabu hiyo mkoani
Mtwara
Na Mwandishi Wetu, Mtwara
WEKUNDU wa Msimbazi, Simba Sc
leo jioni wanacheza mechi ya kirafiki na Ndanda fc katika uwanja wa
Nangwanda Sijaona mkoani Mtwara katika maadhimisho ya Siku ya Ndanda,
‘Ndanda fc Day’. Wakati kikosi cha Simba kikitarajia kutua asubuhi ya
leo Uwanja wa Ndege wa Mtwara kutokea Dar es salaam , jana Rais wa klabu
hiyo, Evans Elieza Aveva akiongozana na mwenyekiti wa
zamani wa klabu hiyo, Hassan Dalali walitua Mtwara kwa ajili ya
maandalizi ambapo kikubwa zaidi alizindua Tawi jipya la Simba mkoani
humu.
Simba jana ilikuwa na mechi ya
pili ya kimataifa ya kirafiki katika uwanja wa Taifa, jijini Dar es
salaam dhidi ya URA ya Uganda na ilifungwa bao 1-0. Wikiendi iliyopita
ilishinda mabao 3-0 dhidi ya Gor Mahia ya Kenya katika mechi ya kwanza
ya kimataifa ya kirafiki.
Wakati Ndanda fc imepanda
Daraja, mtandao huu ulikuwepo katika mapokezi ya timu hiyo hapa Mtwara
ambapo walizindua ‘Slogani’ yao kuwa ‘Ndanda fc kwanza, Simba, Yanga
baadaye’, lakini jana mashabiki hao waligeuka na kusema haiwezekani,
‘Simba kwanza, Ndanda fc baadaye’.
Walipobanwa na mwandishi kwanini
wamegeuka? walijitetea na kusema mechi ya leo ni ya kirafiki ndio maana
wanaishangilia timu yao ya Simba, lakini vijana hao wa Patrick Phiri
wakirudi katika mechi ya ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara watakutana na
mambo mapya na hapo ndipo ‘Ndanda fc itakuwa kwanza, Simba baadaye”.
Raha sana.
Zaidi walisema wamefurahishwa na
ujio wa Rais wao wa kwanza katika Historia ya klabu hiyo, Bwana Aveva,
hivyo wamempokea kwa furaha na wanaandika historia ya kuzindua tawi
jipya.
Msomaji unaweza kupata picha mwenyewe kuhusu namna mashabiki walivyo inapofika Simba na Yanga.
Hapa chini ni baadhi ya picha katika mapokezi ya Aveva na uzinduzi wa tawi…
Jamaa kavalia jezi yenye jina la Emmanuel Okwi: Mambo yalianza mdogo mdogo baada ya Rais wa Simba, Evans Aveva kuwasili mkoani Mtwara akitokea Dar es salaam
Tawi la Mnyama mkoani Mtwara
Umeona nini kwenye picha hii? kuna jamaa kavalia jezi ya timu pinzania, hakuona shida kuwaona watani. Lakini ni ngumu kufahamu, labda kavaa tu kama vazi. Cheki kofia nayo…..
Wamegeuka?: ‘Simba kwanza, Ndanda fc baadaye’., mashabiki wa Simba wakati wa uzinduzi wa tawi la klabu hiyo Mkoani Mtwara
Rais wa Simba (wa pili kulia) wakati wa kusaini kitabu cha wageni kwenye tawi hilo. Wa kwanza kulia ni mwenyekiti wa zamani wa klabu hiyo, Mzee Hassan Dalali.
Rais wa Simba sc, Evans Aveva (wa kwanza kushoto) na Hassan Dalali (wa kwanza kushoto) wakipata msosi kidogo