Published On:Jumanne, 16 Septemba 2014
Posted by Hisia
WELBECK, WILSHERE TAYARI KUIWASHIA MOTO DORTMUND LIGI YA MABINGWA
Jack Wilshere alionekana mwenye morali ya juu
JACK Wilshere
na Danny Welbeck wameonekana kuwa na morali kubwa katika mazoezi ya
Arsenal kujiandaa na mechi ya ligi ya mabingwa inayopigwa leo dhidi ya
Borussia Dortmund.
Wilshere alifunga bao na kuonesha
kiwango cha juu katika sare ya 2-2- na Manchester City, wakati Welbeck
alifurahia kucheza mechi yake ya kwanza na kutolewa baadaye.
Mshambuliaji huyo wa zamani wa
Manchester United alionekana kuimarika na katika mazoezi ya jana Arsene
Wenger alikuwa anampa mazoezi ya kuongeza kasi.

Welbeck (katikati) alicheza dhidi ya Manchester ana ameonekana kuwa imara katika mazoezi ya Arsenal

Arsene Wenger akitoa maelekezo kwa wachezaji wake kuelekea mechi dhidi ya Dortmund itayopigwa leo huko Westfalenstadion