Published On:Alhamisi, 11 Septemba 2014
Posted by Hisia
BAADA YA OKWI, NAO MKATABA WA MBUYU TWITE WAZUA JAMBO, FC LUPOPO WATUA KUDAI CHAO!
USAJILI wa Mbuyu Twite umeingia dosari baada ya
klabu yake ya zamani ya FC Lupopo ya
Congo kuibuka na kusema bado ni mchezaji wake.
Katibu mkuu wa Lupopo, Consntatine Kapika yupo jijini
Dar es salaam kudai fedha zao na wameshangazwa sana na kitendo cha Twite
kusaini mkataba wa mwaka mmoja kuitumikia Yanga baada ya mkataba wa mkopo wa
miaka miwili kumalizika.
Kiongozi huyo alisema viongozi wa Yanga walitakiwa
kuwasiliana na Lupopo kama bado wanamhitaji Twite.
Kapika anajaribu kuwasiliana na viongozi wa Yanga
akiwemo Ahmed Seif ‘Magari’, Abdallah Binkleb na katibu mkuu Beno Njovu, lakini
wanamzungusha bila kupewa nafasi ya kuonana na viongozi wa juu wa Yanga.
Kapika alisema kama Yanga watashindwa kukaa meza
moja na Lupopo, basi nyaraka zote kuhusu mkataba wa mchezaji huyo zitapelekwa
TFF, CAF na hatimaye FIFA.
Taarifa kamili tunaifuatilia kwa kina kutoka pande
zote mbili, Yanga na Lupopo.