Published On:Alhamisi, 11 Septemba 2014
Posted by Hisia
MBEYA CITY FC KUPASHA NA VIPERS SC YA UGANDA JUMAMOSI SOKOINE
MBEYA City fc inatarajia kucheza mechi ya kwanza
ya kimataifa ya kirafiki kujiandaa na msimu mpya wa ligi kuu soka Tanzania bara
dhidi ya Vipers Sc ya Uganda itakayopigwa jumamosi ya wiki hii katika uwanja wa
Sokoine, jijini Mbeya.
Mchana wa leo kocha mkuu wa Mbeya City na kocha
bora wa ligi kuu msimu uliopita, Juma Mwambusi alisema viongozi wa klabu hiyo
walikuwa wanahaha kutafuta mechi ya kimataifa ya kirafiki itayotumika
kujumuisha maandalizi yote na hatimaye kupata kikosi cha kwanza kwa ajili ya
ligi kuu.
Mwambusi alisema maandalizi yanakwenda vizuri na
wachezaji wote wapo katika hali nzuri wakisubiri kufungua kampenzi za msimu
mpya wa 2014/2015 unaotarajia kuanza septemba 20 mwaka na wataanza nyumbani
dhidi ya JKT Ruvu.
Vipers Sc ambayo zamani ilikuwa inaitwa Bunamwaya
kitakuwa kipimo kizuri kwa Mwambusi ambaye ana malengo ya kuwapa changamoto
makocha wenzake wa timu za ligi kuu, hususani Simba, Yanga na Azam fc.
Timu hiyo yenye maskani yake mjini Wakiso, Uganda, inashiriki ligi kuu ya nchi hiyo na inatumia uwanja wa nyumbani wa Bunamwaya wenye uwezo wa kuchukua watazamaji 5,000.