Headlines
Published On:Alhamisi, 11 Septemba 2014
Posted by Hisia

BABA UBAYA, MAGULI HALI TETE SIMBA SC

Issa Rashid (kulia)
BEKI wa Simba Issa Rashid ‘Baba Ubaya’ atalazimika kukaa nje ya uwanja kwa wiki mbili baada ya kuumia nyama za paja kwenye moja ya mazoezi ya klabu hiyo, daktari wa Simba, Yassin Gembe amethibitisha.
Mbali na beki huyo straika Elius Maguli alilazimika kupumzishwa kufanya mazoezi na wachezaji wengine baada ya kuugua Malaria ambapo mpaka jana Jumatano mchana haikufahamika mara moja kuwa angerejea kuendelea na programu hizo siku gani.
Gembe alisema baada ya kwenda kumfanyia vipimo Jumatatu ya wiki hii, Baba Ubaya alishauriwa kukaa nje kwa muda wa wiki mbili wakati Maguli alipumzisha juzi Jumanne kufanya mazoezi na wachezaji wenzake kutokana na kusumbuliwa na Malaria.
“Baba Ubaya atalazimika kukaa nje kwa wiki mbili kuanzia leo (Jumanne) baada ya kugundulika kuwa majeraha yake ya nyama za paja si madogo kama tulivyodhani mwanzo,” alisema Gembe
Majeraha hayo yatamfanya Baba Ubaya kuukosa mchezo wa ufunguzi wa Ligi kati ya Simba na Coastal Union utakaochezwa Jumapili ya Septemba 21.
Chanzo: Mwanaspoti

About the Author

Posted by Hisia on 9/11/2014 12:46:00 PM. Filed under . You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0. Feel free to leave a response

By Hisia on 9/11/2014 12:46:00 PM. Filed under . Follow any responses to the RSS 2.0. Leave a response

0 comments for "BABA UBAYA, MAGULI HALI TETE SIMBA SC"

Leave a reply

    Blog Archive