Published On:Jumanne, 9 Septemba 2014
Posted by Hisia
BILA DIEGO COSTA HISPANIA YAUA 5-1, KINDA JIPYA PACO ALCACER LAIBUA GUMZO!
Ndoto zimeanza: David Silva akimrukia Paco Alcacer wakati akishangilia bao lililowafanya Hispania waongoza 2-0 dhidi ya Macedonia mjini Valencia
HISPANIA wamepata makali tena baada ya
kuifunga 5-1 Macedonia na sasa watazua mjadala kama kweli wanamhitaji
mshambuliaji wa Chelsea, Diego Costa.
Majeruhi ya nyama za paja aliyonayo Costa yalimaanisha mshambuliaji kinda wa Valencia Paco Alcacer aanze katika mchezo wake wa kwanza akiwa na miaka 21.
Nyota huyo anayechipukia alifanikiwa kufunga bao lake la kwanza katika dakika ya 17.
Cesc Fabregas alipiga krosi nzuri iliyomaliziwa na kinda huyo mpya anayevalia jezi namba 9.
Tulia kijana!: Cesc Fabregas akimtoka kiungo wa Macedonian, Stefan Spirovski
Kazi rahisi tu: Sergio Ramos akipongezwa
baada ya kufunga goli kwa mkwaju wa penati katika mchezo wao wa kundi C
uwanja wa Ciutat de Valencia
Anashangilia kimya kimya: Agim Ibraimi alifunga bao la kufutia machozi.
Kikosi cha Spain: Casillas; Alba, Abidol, Ramos (Bartra 68) , Juanfran; Busquets, Silva, Koke (Munir 77), Fabregas, Pedro, Alcacer (Isco 57).
Wafungaji wa magoli: Ramos 16 (pen), Alcacer 17, Busquets 45+3, Silva 50, Pedro 90+1.
Kadi ya njano: Koke, Fabregas.
Kikosi cha Macedonia: Pacovski,
Cuculi, Sikov, Mosjsov, Alioski (Demiri 46), Trajkovski, Spirovski
(Radeski 64), Ristovski, Abdurahimi (Velkoski 74), Jahovic, Ibraimi.
Mfungaji wa goli: Ibraimi 28 (pen).
Kadi ya njano: Ristovski, Abdurahimi.