Published On:Jumamosi, 20 Septemba 2014
Posted by Hisia
EVERTON YAANZA VYEMA EUROPA LEAGUE, YAWAFUMUA WAJERUMANI 4-1
KLABU ya 
Everton ya England imeanza vyema michuano ya Europa League baada ya 
kuichapa Wolfsburg ya Ujerumani manbao 4-1 Uwanja wa Goodison Park.
Kikosi cha Roberto Martinez kilionyesha ni moto tangu mapema tu kwenye mchezo huo, baada ya
Ricardo Rodriguez kujifunga mapema tu akijaribu kuokoa shuti la Steven Naismith kuipatia Everton bao la kuongoza. 
Seamus 
Coleman akafunga la pili karibu na mapumziko na Leighton Baines 
aliyechangia mabai yote ya awali, akafunga la tatu kwa penalti baada ya 
Aiden McGeady kuchezewa faulo. 

Kevin 
Mirallas akafunga bao la nne dakika za mwishoni kabla ya Rodriguez 
kuwafungia wageni bao la kufutia machozi kwa mpira wa adhabu wa dakika 
ya mwisho.
Kikosi 
cha Everton kilikuwa; Howard, Coleman/Osman dk90, Stones, Jagielka, 
Baines, Barry, McCarthy, McGeady, Naismith/Gibson dk82, Mirallas na 
Lukaku/Eto’o dk69. 
Wolfsburg:
 Benaglio, Jung, Knoche, Naldo, Rodriguez, Luiz Gustavo/Guilavogui dk77,
 Malanda/Hunt dk46, De Bruyne, Arnold, Caligiuri/Bendtner dk60 na Olic.








 
 
 
 
 
 
