Published On:Jumamosi, 20 Septemba 2014
Posted by Hisia
PIGO ARSENAL, DEBUCHY KUWA NJE KATI YA WIKI SITA HADI MIEZI MITATU
BEKI wa
pembeni wa Arsenal, Mfaransa Mathieu Debuchy anaweza kuwa nje ya Uwanja
hadi Krisimasi baada ya kuumia enka dhidi ya Manchester City mwishoni
mwa wiki iliyopita.
Kocha
Arsene Wenger amesema kwamba Debuchy alitarajiwa kwenda kufanyiwa
uchunguzi kama atahitaji upausaji wa kifundo chake cha mguu jana jioni
ambao utatoa majibu atakaa nje kwa muda gani.
Ikiwa
hatahitaji upasuaji, itamchukua wiki sita nje ya Uwanja kabla ya kurejea
dimbani, lakini kama atapigwa 'kisu' atakuwa nje kwa angalau miezi
mitatu.
Mathieu Debuchy akiugulia maumivu baada ya kuumia wiki iliyopita dhidi ya Manchester City