Headlines
Published On:Jumanne, 16 Septemba 2014
Posted by Hisia

JAMIE CARRAGHER ADAI ARSENAL HAWAWEZI KUNYANYUA KOMBE LA LIGI KUU


Jamie Carragher usiku wa jana alidai kuwa Arsenal haiwezi kushinda taji la ligi kuu.

JAMIE Carragher anaamini Arsenal hawatashinda ubingwa msimu huu baada ya kushindwa kulinda bao la kuongoza dhidi ya Manchester City jumamosi iliyopita.
Bao la dakika ya 83 la Martin Demichelis lilifanya mechi imalizike kwa sare ya 2-2 katika uwanja wa Emirates.
Kwa matokeo hayo, maana yake tayari Arsenal wameshatoa sare katika mechi zao tatu za ligi kuu na kuachwa nyuma kwa painti sita na vinara Chelsea. 
Beki wa zamani wa Liverpool, Carragher amesema Arsenal imekuwa nyuma sana dhidi ya Chelsea msimu huu kama ilivyokuwa mwaka jana.
Akizungumza na Sky Sports, Carragher alisema: "Nilizungumza mwanzoni mwa msimu, sidhani kama Arsenal watashinda ubingwa. Ninavyoiona Arsenal ni sawa na Chelsea ambapo moja ilimaliza nafasi ya tatu na nyingine ya nne. Yawezekana walitumia kiasi cha fedha kinachoelekea majira ya kiangazi.
"Kwanini Arsenal haikumpata [Diego] Costa. Danny Welbeck anaweza kuwa usajili mzuri. Wanahitaji beki wa kushoto, Chelsea walienda Atletico Madrid na kumpata Felipe Luis. Wanafanya kila wanachotaka kufanya".
Arsenal walipata changamoto ya kuingia nne bora msimu uliopita na Carragher anaamini washika bunduki hao wa London hawawezi kutwaa taji msimu huu.
Martin Demichelis equalised for Manchester City late on to rescue a 2-2 draw at Arsenal on Saturday
Martin Demichelis aliifungia bao la kusawazisha Manchester na kuipa sare ya 2-2- dhidi ya Arsenal siku ya jumamosi
Jack WIlshere's fabulous strike had put the Gunners 2-1 up at the Emirates Stadium
Jack WIlshere aliifungia Arsenal bao zuri 

About the Author

Posted by Hisia on 9/16/2014 07:08:00 PM. Filed under . You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0. Feel free to leave a response

By Hisia on 9/16/2014 07:08:00 PM. Filed under . Follow any responses to the RSS 2.0. Leave a response

0 comments for "JAMIE CARRAGHER ADAI ARSENAL HAWAWEZI KUNYANYUA KOMBE LA LIGI KUU"

Leave a reply

    Blog Archive