Published On:Jumanne, 16 Septemba 2014
Posted by Hisia
PAUL SCHOLES AWAFAGILIA WEKUNDU WA ANFIELD LIVERPOOL
Brendan Rodgers akiwapa mbinu wachezaji wake kuelekea katika mchezo wa kundi B wa ligi ya mabingwa.
MSHINDI wa ligi ya mabingwa ulaya,Paul
Scholes anaamini kuwa Liverpool wanaweza kutoa upinzani mkali katika
mashindano ya mwaka huu.
Liverpool, mabingwa mara tano wa ulaya wamerudi tena katika michuano hiyo msimu huu baada ya kukosekana kwa miaka mitatu.
Majogoo hao wa jiji wanaanza kampeni yao leo jumanne kwa kuwakaribisha mabingwa wa Bulgaria, Ludogorets.
Pia watachuana na mabingwa watetezi Real Madrid na wakali wa Uswizi , Basle katika michezo ya kundi B.
Scholes aliyekuwepo katika kikosi cha
Manchester United kilichotwaa ubingwa mwaka 2008, anatarajia kuona
Anfield inakuwa sehemu ngumu kwa timu zitakazotua hapo.
Mkongwe huyo aliyasema hayo wakati akichambua ligi ya mabingwa katika kituo cha ITV.
Scholes alisema: "Liverpool ni farasi weusi katika michuano ya mwaka huu.
"Brendan Rodgers amefanya kazi kubwa.
Staili ya uchezaji aliyochagua inavutia kuitazama na wachezaji
wameonekana kumuelewa. Nahisi watafanya vizuri tena kwa aina ya
wachezaji walionao".
"Faida kubwa kwao ni mashabiki wa
nyumbani. Anfield ni sehemu inayotisha kwenda wakati wote, kitu ambacho
Manchester City wamekosa"
Bosi wa Liverpool , Brendan Rodgers anatarajia kutumia faida ya mashabiki wa Anfield.
Liverpool walifanikiwa kufuzu UEFA baada
ya kuonesha kiwango kikubwa msimu wa 2013/2014 wa ligi kuu England,
lakini wakaishia kushika nafasi ya pili dhidi ya Manchester City.
Wamempoteza nyota wao Luis Suarez
aliyejiunga na FC Barcelona, lakini Scholes anaamini Mario Balotelli
anaweza kurithi nafasi hiyo.
Akimzungumzia Suarez, Scholes alisema:
"Ni mchezaji mkubwa, lakini usisahau kuwa wamemsajili Balotelli, anaweza
kuwa mshindi wa mechi pia".