Headlines
Published On:Jumanne, 16 Septemba 2014
Posted by Hisia

KOCHA WA AZAM FC ABWAGA MANYANGA.


Aliyekuwa Kocha mkuu wa Azam Acadamy Vivik Nagul amepata timu ya ligi kuu India.
Ikiwa ni siku kadhaa zimepita tangu Azam FC ipoteze mchezo wa ngao ya Jamii mbele ya Yanga kwa kipigo cha bao 3-0, Kocha mkuu wa Azam Academy Vivik Nagul ameachana na wanalamba lamba hao na kutimkia India kuinoa klabu ya ligi kuu.
Akizungumza na mwandishi wetu Afisa habari wa Azam FC Jafari Idd Maganga amesema kuwa Kocha huyo raia wa India baada ya kupata timu hiyo huku kwao aliomba uongozi uweze kumruhusu kujiunga nao katika ajira mpya na kama uongozi wakawa hawanabudi kumpa baraka zote.
“Ni kweli tayari Kocha amekwisha ondoka nchini kuelekea India ambako ni nyumbani kwao baada tu ya kumalizana naye kwa kila kitu, huko amepata timu inayo shiriki ligi kuu na anakwenda kuwa kocha mkuu” Amesema Jafari Idd.
“Ni kocha mzuri ambaye tulikuwa naye toka enzi za John Stowert Hall ambaye walikuwa wakifanya kazi wote Uingereza ndipo akajiunga nasi, Ametupatia mafanikio makubwa sana hivyo hatuna budi kumpa hishima yake” Ameongeza Jafari Idd
Kutokana kocha huyo Muindi kutimkia kwao mikoba yake ya kuinoa Azam Academy inatazamiwa kukabidhiwa Kwa Watanzania Nyota wa Soka la Bongo wa zamani Mfumania Nyavu Phiripo Alando ambaye pia amewahi kuichezea Azam FC au kwa beki kisiki wa zamani Idd Tcheche.
“Yeah ni kweli kabisa nafasi haiwezi kubaki wazi, lakini alikuwa na viongozi wa karibu kama Alando pamoja na Tchetche hawa ndio wanaweza kukabidhiwa Academy mmoja wapo” Amesema Jafar Idd.
Philipo Alando anayetazamiwa kukabidhiwa mikoba ya Vivik Nagul wakiwa pamoja
Philipo Alando anayetazamiwa kukabidhiwa mikoba ya Vivik Nagul wakiwa pamoja
Nagul aliiongoza Azam FC kwa mara ya mwisho katika mchezo wa utangulizi wa Ngao ya Jamii dhidi ya Azam, Academy ikiwafunga watoto wa Yanga mabao 2-0 Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Nagul atakumbukwa Azam FC kwa kazi yake nzuri baada ya kuweza kuzarisha wachezaji nyota na tegemezi katika klabu na timu za Taifa U17-U20 kama Joseph Kimwaga, Aishi Manula, Kevin Friday, Farid Mussa, Gariel Michael na wengineo.
Aliiwezesha Azam Academy kutwaa mataji kadhaa kama Kombe la Uhai na Rollingtosn pamoja na pia kuwa tegemeo la timu za taifa za vijana nchini kwa wachezaji wengi wanaozalishwa hapo kuchukuliwa timu za kuanzia U17 hadi U20.
Taji lake la mwisho ambalo ameipatia Azam FC ni kikombe cha Rollingstone ambaco alikibeba mwezi jana katika uwanja wa Karume ikiwa ni kwa mara ya kwanza wakinyakua kikombe hicho.
Idd Tchetche anayetazamiwa kukabidhiwa academy.
Idd Tchetche anayetazamiwa kukabidhiwa academy.

About the Author

Posted by Hisia on 9/16/2014 07:40:00 PM. Filed under . You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0. Feel free to leave a response

By Hisia on 9/16/2014 07:40:00 PM. Filed under . Follow any responses to the RSS 2.0. Leave a response

0 comments for "KOCHA WA AZAM FC ABWAGA MANYANGA. "

Leave a reply

    Blog Archive