Published On:Jumamosi, 13 Septemba 2014
Posted by Hisia
MARCIO MAXIMO ATAMBA KIKOSI CHA YANGA KAMILI GADO KUIVAA AZAM FC NGAO YA JAMII
Kikosi cha Young Africans Sports Club
Na Mwandishi Wetu, Dar es salaama
PAZIA la
Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania bara litafunguliwa kesho kwa mchezo wa Ngao ya
Jamii kwa Young Africans kucheza na timu ya Azam FC kwenye dimba la Uwanja wa
Taifa kuanzia majia ya saa 10:00 jioni kwa saa za Afrika Mashariki.
Young
Africans ambayo imekua na rekodi ya kufanya vizuri katika michezo ya Ngao ya
Jamii, itashuka dimbani kupambana na wana lambalamba Azam FC huku ikiwa na
kumbumbuku ya ushindi katika mchezo wa Ngao ya Jamii msimu uliopita ambapo
watoto wa Jangwani waliibuka na ushindi wa bao 1-0, mtikisa nyavu akiwa ni
Salum Telela "Essien".
Kocha
Marcio Maximo ambaye atakua akiongoza Yanga mara ya pili katika dimba la Uwanja
wa Taifa amesema vijana wake wote wapo katika hali nzuri jambo ambalo linampa
wigo mpana wa kikosi kuchagua nani amtumie katika mchezo huo.
Mpaka
sasa Maximo ameiongoza Yanga katika michezo minne ya kirafiki akifanikiwa
kushinda michezo yote ambapo aliibuk ana ushindi 1-0 (Chipukizi FC), 2-0
(Shagani FC), 2-0 (KMKM) na 1-0 (Thika United) kutoka nchini Kenya.
Katika
mazoezi ya mwisho yaliyofanyika leo asubuhi katika Uwanja wa shule ya Sekondari
Loyola mchezaji pekee ambaye hakuweza kufana mazoezi ni Jerson Tegete
anayesumbuliwa na nyonga, huku mbrazil Coutinho akifanya mazoezi mepesi chini
ya usimamizi wa daktari wa timu Dr. Suphian Juma.
Wapenzi
wa Young Africans mnaombwa kujitokeza kwa wingi kesho kuja kuwashangilia vijana
katika mchezo huo, kwani kocha mkuu mbrazil Maximo ameliandaa jeshi lake lote
kupambana na kupata ushindi kwenye mchezo.
Jumla ya
wachezaji 26 wameendelea kuwepo kambini kujiandaa na mchezo huo katika Hoteli
ya Tansoma iliyopo eneo la Gerezani - Kariakoo :
Wachezaji
waliopo kambini ni:
Walinda mlango: Juma Kaseja, Ally Mustafa "Barthez" na Deo Munish
"Dida"
Walinzi wa Pembeni: Juma Abdul, Salum Telela, Oscar Joshua, Edward Charles na Amos
Abel
Walinzi wa kati: Kelvin Yondani, Rajab
Zahir, Pato Ngonyani na Nadir Haroub "Cannavaro"
Viungo: Mbuyu Twite, Hassan
Dilunga, Omega Seme, Hamis Thabit, Nizar Khalfani, Haruna Niyonzima na Said
Juma "Makapu"
Washambuliaji: Saimon Msuva, Mrisho Ngasa, Huseesin Javu, Said Bahauzi, Andrey
Coutinho, Geilson Santana "Jaja" na Hamis Kizza
"Diego"
Tayari TFF ilishatangaza viingilio vya
mchezo huo kuwa ni Tshs 30,000 (VIP A) Tshs 20,000 (VIP B & C) Tshs 10,000
(Rangi ya Chungwa) na Tshs 5,000 (Bluu & Kijani).
Ununuaji
wa tiketi unafanyika kwa huduma ya M-PESA au wakala CRDB Fahari Huduma