Published On:Jumatano, 10 Septemba 2014
Posted by Hisia
STAND UNITED YALAMBA MILIONI 10 ZA UDHAMINI KUTOKA BENKI YA EXIM
BENKI ya Exim
Tanzania imeingia mkataba wa udhamini wa mwaka mmoja na klabu ya Stand
United inayojiandaa kushiriki ligi kuu soka Tanzania bara msimu wa 2014/2015
unaotarajia kuanza septemba 20 mwaka huu.
Stand United yenye makao makuu yake Mkoani Shinyanga itaanza
kampeni zake nyumbani kwa kuvaana na wageni wenzao wa ligi kuu, Ndanda fc
kutoka Mtwara.
Taarifa zinaeleza kuwa katika mkataba hao, Stand United
watalamba milioni 10 za Kitanzania.
Huu ni udhamini wa nne kwa klabu hiyo kwani tayari walishalamba
udhamini wa kampuni ya Binslum sambamba na klabu za Mbeya City na Ndanda fc ya
Mtwara ,Azam Tv na wadhamini wakuu wa ligi, kampuni ya Simu za mkononi, Vodacom
Tanzania.
Kwa maana hiyo, Stand United watakuwa wanakusanya fedha za
udhamini kutoka Binslum, Azam TV na Benki ya Exim.
Mkataba wa Exim na Stand United unahusisha kuweka mabango
ya benki hiyo uwanjani, nembo kwenye gari la timu na kwenye jezi. Pia
kuweka bango nyuma ya mikutano ya viongozi au makocha wakati wanazungumza na
waandishi wa habari.
Hivi karibuni wachezaji wa Stand United waliripotiwa kugoma
kufanya mazoezi wakishinikiza kulipwa mishahara, lakini uongozi ukafafanua kuwa
kuna mahali kulitokea tatizo na fedha zipo.
Viongozi hao walikiri kufanya uzembe na walifanikiwa kumaliza
tatizo.
Kwa udhamini huu, Stand United watakuwa na uwezo wa kufanya
mambo ya msingi klabu kwao.