Published On:Jumatano, 10 Septemba 2014
Posted by Hisia
John Bocco Kukosa Mechi 3 za Mwanzo wa Ligi kuu bara(VPL) pamoja na Ngao ya Hisani Jumapili dhidi ya Yanga
NJE
WIKI TATU! Captain John Bocco pamoja na jana kufanya mazoezi katika
Gym ya kisasa pale Chamazi - Azam Complex, lakini vipimo alivofanyiwa
mchana na mtaalamu (physiotherapist) Gilbert Kigade pale Msasani
Peninsula Hospital ili kuangalia maendeleo yake, alibainisha kwamba
Bocco anatakiwa apumzike kwa wiki 3 huku akipata matibabu. Bocco
anasumbuliwa na maumivu ya misuli na hivyo ataikosa mechi ya
Jumapili dhidi ya Yanga na pia michezo 3 ya mwanzo ya Ligi kuu ya
Vodacom.