Published On:Alhamisi, 11 Septemba 2014
Posted by Hisia
YANGA WAINGIA CHIMBO KUIWINDA AZAM FC, TEGETE BADO MZIMU WA MAJERUHI WAMUANDAMA!
KIKOSI cha Brazil, Marcio Maximo kimeingia kambini
jioni ya leo kujiandaa na mechi ya Ngao ya Jamii dhidi ya Azam fc itayopigwa jumapili
(septemba 14 mwaka huu) uwanja wa Taifa jijini Dar e salaam .
Kambi hiyo ya Yanga imewekwa katika Hoteli ya
Tansoma iliyopo eneo la Gerezani, jijini Dar es salaam.
Imeripotiwa kuwa mshambuliaji wa klabu hiyo,
Brazil Andrey Coutinho aliyeumia katika mechi ya kirafiki jana asubuhi dhidi ya
Polisi Dar katika uwanja wa shule ya sekondari Loyola, Mabibo, Dar es salaam naye
ameingia kambini na anaendelea na matibabu.
Coutinho hali yake inaendelea vizuri na leo
alifanya mazoezi ya Gym, lakini kuhusu kucheza au kutocheza mechi hiyo ya
jumapili taarifa bado haijatolewa kutoka kwa jopo la madaktari.
Naye Jeryson John Tegete ameripotiwa kutoingia
kambini kutokana na kusumbuliwa na majeruhi ya nyonga.
Kwa takribani misimu miwili sasa, Tegete hajawa
fiti sana kwani alikuwa anasumbulia na majeruhi ya goti kwa muda mrefu, lakini
mwishoni mwa msimu uliopita alitumika na kuonesha kiwango cha juu.
Achalia mbali wachezaji hao wawili wanaosumbuliwa
na majeruhi, wengine wote wako fiti na wameingia kambini kunoa makali.
Awali iliripotiwa Yanga wangejichimbia Bagamoyo mkoani Pwani kama walivyokuwa wanafanya msimu uliopita, lakini wameamua bora wajifiche hapa hapa Dar.