Published On:Alhamisi, 11 Septemba 2014
Posted by Hisia
ANGALIA KUFURU HII YA NDEGE MPYA YA WANAMICHEZO, NIKE INASHIRIKI UTENGENEZAJI WAKE

Kampuni moja ya ndege
imeamua kutengeneza ndege maalum kwa ajili ya wanamichezo ili kuwasaidia
kutokana na uchovu.
Inaaminika
wanamichezo wamekuwa katika uchovu mkubwa kutokana na safari nyingi za
ndege kwenye klabu ikijumuishwa na timu zao za taifa.
Kutokana
na hali hiyo kampuni ya vifaa vya michezo ya Nike imeamua kushirikiana
na kampuni hiyo ya ndege ambayo haijatajwa kupata ndege ambayo itakuwa
na sehemu maalum kwa ajili ya wanamichezo ambayo itawapunguzia uchovu
licha ya safari ndefu.

Imetolewa
mfano wachezaji wa Brazil ambao walirejea kwao kuungana na timu yao,
halafu ikafunga safari hadi Marekani ilipocheza mechi za kirafiki na
sasa watarejea kwenye timu zao Ulaya watasafiri zaidi ya kilomita 8000.
Wachezaji wa Premier League, La Liga, Serie A, Bundesliga ndiyo wanaoongoza kwa safari ndefu.
Ndani
ya ndege hiyo kutakuwa kuna sehemu ya kupumzikia, kulala, kucheza
michezo mbalimbali na vitu vya aina yake vitakavyopunguza uchovu.

Maana
yake wachezaji wa Ligi Kuu Bara (Tanzania), hawatapata nafasi ya
kupanda ndege hizo kwa kuwa hata ndege za kawaida tu, ni timu chache
labda za Yanga, Simba, Azam FC na Mbeya City zimekuwa zikipata nafasi ya
kusafiri kwa ndege za kawaida.
Kingine
timu hizo hazina safari ndefu sana kwa kuwa timu ni 14 tu, hivyo
kuifanya kila moja kucheza mechi 28 kwa msimu na mechi nyingi zinachezwa
jijini Dar.

