Published On:Alhamisi, 11 Septemba 2014
Posted by Hisia
MECHI YA COASTAL UNION NA MTIBWA SUGAR YASOGEZWA MBELE SASA KUCHEZWA JUMAPILI
Na Mwandishi Wetu, Tanga
TIMU
ya Coastal Union ya Tanga “Wagosi wa Kaya” ambayo ilikuwa icheze mechi
ya kirafiki na Mtibwa Sugar Jumamosi wiki hii kwenye uwanja wa CCM
Mkwakwani mchezo huo umesogozwa mbele sasa kucheza Jumapili katika
Uwanja wa Mkwakwani ikiwa ni maandalizi ya kuelekea msimu mpya wa ligi
kuu soka Tanzania bara ambao unatarajiwa kuanza Septemba 20 hapa nchini.
Mchezo huo umesogezwa mbele kwa sababu ya kuwepo kwa mechi za uingereza Jumamosi
Akizungumza leo,Ofisa
Habari wa Coastal Union,Oscar Assenga amesema maandalizi ya kuelekea
mchezo huo yanaendelea vizuri na tayari walishafanya mazungumzo na
uongozi wa wakata miwa hao hivyo watawasili mkoani hapa siku moja kabla
ya mchezo huo.
Assenga
amesema kuwa mchezo huo utakuwa ni wa pili kwa timu ya Coastal Union
kucheza ikiwa mkoani hapa baada ya kurejea kutoka Visiwani Pemba
ilipokuwa imeweka kambi ya mwezi mmoja kwa ajili ya matayarisho ya ligi
kuu soka Tanzania bara.
Amesema
baada ya mchezo wa kwanza timu hiyo kuibuka na ushindi wa mabao 2-0
dhidi ya Polisi Morogoro hivyo waliona umuhimu wa mechi hiyo lengo
likiwa kukipa makali kikosi hicho kabla ya kuwavaa wekundu wa msimbazi
Simba siku ya ufunguzi wa Ligi kuu.
Ameongeza
kuwa wanategemea mechi hiyo itakuwa na upinzani mkubwa sana hivyo
wakazi wa Tanga na vitongoji vyake watumia fursa hii kuja kuiona timu
yao ya Coastal Union ikipambana kwenye mchezo huo kabla haijaanza msimu
mpya wa ligi kuu Tanzania bara
Hata
hivyo amesema kuwa msimu huu timu hiyo imepania kuhakikisha inafanya
vizuri katika mechi zake za nyumbani na ugenini ili kuweza kuchukua
ubingwa wa Ligi kuu Tanzania bara .