Published On:Jumanne, 9 Septemba 2014
Posted by Hisia
Villa Squad kukipiga na Ashanti United kesho Jumatano
NA ANDREW
CHALE
TIMU ya
Daraja la Kwanza ya Villa Squad ya Magomeni, Dar es Salaam, siku ya Jumatano Septemba 10 inatarajia kushuka dimbani
kucheza mchezo wa kirafiki na timu ya Ashanti United ‘Wauza mitumba, ya Ilala
mchezo utakaochezwa uwanja wa Mwananyamala shule.
Kwa mujibu
wa Katibu wa Villa, Mbarouk Kasanda mchezo huo utakuwa ni mahususi kwa ajili ya
kukipa makali kikosi chao hicho kinachotarajia kujiwinda kurejea ligi kuu msimu
ujao.
Kasanda
aliwaomba marafiki wa Villa na wadau wa
soka Kinondoni kujitokeza kwa wingi uwanja
wa shule ya Msingi Mwananyamala kushuhudia timu hiyo yenye wachezaji mbalimbali
wakiwemo walioachwa na timu kubwa zikiwemo za Simba, Yanga, Azam, Mtibwa na Coastal
Union.
Mcheazo huo
unatarajiwa kuwa mkali kwa timu zote mbili, kutokana na kukamiana kila
wanapokutana, ikiwemo zilipokuwa ligi kuu misimu iliyopita. Kiingilio cha mchezo huo kinatarajiwa kuwa sh 1,000.
Kwa upande
wake, Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili wa Villa, Idd Godgod alisema
wameamua kujipanga kuakikisha wanarejea ligi kuu ndio maana wamesajili
wachezaji wakongwe na wazoefu sambamba na kuchanganya damu changa.
Godgod
aliwataja baadhi ya wachezaji waliowasajili chini ya ufadhili wa mdau wa soka, Nassoro
Binslum, ni pamoja na Ramadhani Chombo ‘Redondo’ aliyeachwa na Simba, Ibrahim
Mwaipopo kutoka Azam FC na Ally Mohamed ‘Gaucho’ (Mtibwa Sugar) ya Morogoro.
Wengine ni Nurdin Bakari, Godfrey Taita, Pius
Kasambale,Jamal Magulu, Rashid Roshuwa na wengine wengi ambao kwa sasa bado
wanasubiria hatua ya mwisho kuwaweka wazi.
Pia
timu hiyo inatarajia kuendelea na mazoezi yake uwanja wa Muhimbili
chini ya kocha wao, Kamba Lufu ambapo wadau mbalimbali wameombwa
kujitokeza kuipa sapoti timu hiyo.