Published On:Jumamosi, 20 Septemba 2014
Posted by Hisia
JOSE MOURINHO AIBUA CHOKOCHOKO CHELSEA IKISAFIRI KUIFUATA MAN CITY ETIHAD
Jose Mourinho amedai kuwa klabu
zinazoshindwa kufuata sheria ya matumizi ya fedha ziondolewa katika
michuano ya ligi ya mabingwa
JOSE Mourinho ameibwatukia Manchester
City wakati huu Chelsea akijiandaa kusafiri kwenda Etihad, akidai kuwa
UEFA lazima ichukue pointi na kuinyang`anya ubingwa timu inayoshindwa
kufuata sheria ya matuzimi ya fedha (FFP).
Bosi huyo wa Chelsea alisema adhabu hiyo
itakuwa ya haki zaidi kuliko ya sasa ya kutoza faini na kuizuia klabu
kusajili kama ilivyowakumba City.
"Kila mtu anajua kuwa kuna faini, na
kama faini zipo, njia za kuzuia zinakuwepo," alisema Mourinho. "Lakini
faini hizo ni za haki? sidhani. Kwa maoni yangu, kitu cha kwanza ni
kuondoa pointi na kuondoa ubingwa"
James Milner na Martin Demichelis
wakimkaba Arjen Robben wakati wa mechi ya UEFA ambapo Manchester City
ilitandikwa bao 1-0 na Bayern Munich
"Kama una mtaji ambao unakufanya umalize
tatizo la FFP; halafu unashinda makombe na kutozwa faini, utaendelea
kufanya kitu hicho hicho".
Mourinho aliongeza kuwa: "Watamtoa
mchezaji mmoja au wawili katika orodha ya UEFA. Halafu badala ya
wachezaji 24 unakwenda na wachezaji 22. Lakini kama inaelezwa kuwa
utaanza msimu ujao wa UEFA ukiwa umekatwa pointi sita au hutacheza
michuanoo ijayo ya UEFA na utakwenda michuano ya Europa, itaonekana kuwa
na nguvu'
UEFA waliziadhibu City, Paris Saint-German na Zenit St Petersburg kwa kuvunja sheria ya FFP mwaka huu.
City walitozwa faini ya paundi milioni
50 ingawa inaweza kupunguzwa kama wataifuata baadaye na kikosi chao
kinachocheza UEFA mwaka huu kimepunguzwa mpaka wachezaji 21.