Published On:Ijumaa, 12 Septemba 2014
Posted by Hisia
MAFUNZO YA TIKETI ZA ELEKTRONIKI UWANJA WA TAIFA
Shirikisho
la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kesho Jumamosi (Septemba 13 mwaka huu)
saa 4 asubuhi litaendesha mafunzo ya matumizi ya tiketi za elektroniki
kwa wadau wa mpira wa miguu Dar es Salaam.
Mafunzo
hayo Uwanja wa Taifa, na kushirikisha wasimamizi wa mechi, viongozi wa
Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) na makatibu na
maofisa habari wa klabu za Azam na Yanga.
Washiriki
wengine wa mafunzo hayo ni Meneja wa Uwanja wa Taifa na msaidizi wake,
wasimamizi wa milangoni (stewards), waandishi wa habari wa Dar es Salaam
maofisa usalama wa TFF.
Mafunzo
hayo yatahitimishwa Jumapili (Septemba 14 mwaka huu) kwa mechi ya Ngao
ya Jamii kati ya Azam na Yanga kuanzia saa 10 kamili jioni. Tiketi
zimeanza kuuzwa jana (Alhamisi) kupitia M-Pesa, CRDB Simbanking na
maduka ya Fahari Huduma.
BONIFACE WAMBURA
MKURUGENZI WA MASHINDANO
SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)