Published On:Jumapili, 14 Septemba 2014
Posted by Hisia
NSSF YADHAMINI PAMBANO LA SIMBA NA NDANDA FC MKOANI MTWARA
NSSF
kupitia mpango wake wa Wakulima Scheme yadhamini mechi ya kujipima nguvu
kati ya Simba ya Dar es Salaam na Ndanda FC ya Mtwara kwenye uwanja wa
CCM wa Nangwanda Sijaona na kuhudhuriwa na maelfu ya washabiki wa soka
mkoani Mtwara.
Mchezo
huo pia ulikuwa ni sehemu ya sherehe za Ndanda Day ulihudhuriwa na
viongozi mbali mbali wakiwemo wa Serikali uliisha kwa matokeo ya timu
hizo kutoka suluhu.
NSSF
kupitia mpango maalum wa wakulima schemes wenye lengo la kuandikisha na
kuhudumia wakulima kwenye mfuko ya hifadhi ya jamii nchini ili
kuwawezesha wakulima wote nchini wawe kwenye mfuko wa huo kupata
pensheni ya uzeeni pindi watakapo fikisha umri wa miaka 55 na kuendelea
wakulima hao wataweza kulipwa penshion zao hadi watakapo fariki.
Mpangu
huu unamwezesha mkulima kupitia chama cha wakulima AMCOS kuweza kupata
mkopo na taarifa muhimu kuhusu wakulima,wakulima wanachama wa NSSF
wanajiunga bure na kuchangia kuazia shilingi 20,000 na kuendelea.
Aidha
mpangu huu unampa mkulima nafasi pekee ya kulipa kwa msimu wa mavuno
yaani msimu wa mavuno anaweza kulipia kwa mwaka mzima, miezi anayoweza
lipia, lakini pia wakulima wanaweza lipia baada miezi iliyopitilizia
bila malipo msimu wa mavuno.
NSSF
likiwa ni shirika pekee lenye kuwapa huduma ya afya bure wanachama na
kuwawezesha wanachama kutoyumba kiuchumi kwa sababu za gharama za
matibabu kwenye familia.
NSSF
linawahudumia familia ya mwanachama kwa kuwapa matibabu bure watoto
wanne mwanachama na mwenza.matibabu haya wanapata pia wakulima
wanaojiandikisha kwenye mpango huu wa SHIB wa NSSF na kuwawezesha
kuokoa vipato vyao ambavyo vingetumia kwenye matibabu.
NSSF
mkoa wa mtwara unampango wa kuandikisha wanachama 63,000 kutoka kwa
wakulima wa vijiji na wilaya zote mkoani mtwara ambazo ni
Tandahimba,Nanyumbu,Masasi ,Nachingwea,Newala,Mtwara Vijijini ambao
wengi ni wakulima wa zao korosho.
Pia
kwa akina mama wanapata mafao ya uzazi,kabla na baada ya
kujifungua.aidha wakuliwa wataweza kupata mikopo kupitia SACCOS zao na
kuwawezesha kununua mbolea,madawa ya kuulia wadudu,pembejeo,dhana mbali
mbali za kilimo ili kujiinia kiuchumi kupitia NSSF SACCOS Loans.
Ofisi
ya NSSF Mkoa wa Mtwara umeshatoa jumla ya shilingi Bilion 1.75 kwa
SACCOS zilizokidhi vigezo na kuwainua kimaisha wajasiriamali, wakulima
na wafanyakazi.
Wachezaji
wa Simba na Ndanda FC wakiingia Uwanjani wakati wa
mchezo wa maalum wa kusherehekea Ndanda Day uliofanyika leo kwenye
Uwanja wa Nangwanda Sijaona mjini Mtwara na kudhaminiwa na Shirika la
Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF),
kupitia mpango wake wa Wakulima Scheme. Timu hizo zilitoka suluhu. (Na
Mpiga
Picha Wetu)
Mkuu
wa Mkoa wa Mtwara Kanali mstaafu Joseph Simbakalia akisalimia na timu
ya Ndanda FC kabla ya mchezo wao na timu ya Simba uliofanyika leo kwenye
Uwanja wa
Nangwanda Sijaona mjini Mtwara.
Mkuu
wa Mkoa wa Mtwara Kanali mstaafu Joseph Simbakalia akikagua timu ya
Simba wakati wa mchezo wa kirafiki na timu ya Ndanda FC uliofanyika leo
kwenye Uwanja wa Nangwanda Sijaona mjini Mtwara.
Kikosi kamili cha timu ya Simba kilichopambana na Ndanda FC.
Kikosi cha Ndanda FC kikiwa klatika picha ya pamoja kabla ya pambano lao na Simba.
Wachezazaji wa Simba na Ndanda wakichuana katika uwanja wa Nangwanda Sijaona.
Mashabiki wa soka wakifuatilia pambano la Simba na Danda FC.