Published On:Jumatano, 17 Septemba 2014
Posted by Hisia
TEVEZ BADO MOTO, APIGA ZOTE MBILI JUVE IKIUA 2-0 ULAYA,
MABAO mawili ya mshambuliaji wa zamani wa Manchester United, Muargentina Carlos Tevez usiku huu yameipa ushindi wa 2-0 Juventus ya Italia katika mchezo wa makundi Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Tevez
aliyewahi pia kuchezea Manchester City, alifunga bao moja kila kipindi
dhidi ya Malmo FF ya Sweden katika dakika za 59 na 90 na kukipa mwanzo
mzuri Kibibi Kizee cha Turin katika michuano hiyo mikubwa zaidi ya klabu
barani Ulaya.
Wana fainali wa michuano ya msimu uliopita, Atletico Madrid wamepata kipigo cha ugenini kutoka kwa Olympiacos ya Ugiriki cha mabao 3-2.
Mabao ya wenyeji yamefungwa na Arthur Masuaku dakika ya 13, Ibrahim Affelay dakika ya 31 na Mitroglou dakika ya 74 wakati ya wageni yamefungwa na Mario Mandzukic dakika ya 38 na Griezmann dakika ya 87.